Kumkana Mungu au kukataa kumwamini Yesu Kristo, si uhakika wa mtu kusonga mbele kimaendeleo, bali huwa chanzo cha umaskini wa kiroho na kimaadili, ambao umekuwa ni sifa ya Ulaya kwa nyakati zetu. Na ikiendelea kwa muda mrefu, hutengeneza utamaduni wa umaskini miongoni mwa jamii si kiroho tu lakini hata kiuchumi pia. Ni ujumbe kutoka Mkutano wa kwanza wa Baraza la Marais wa Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya. Ujumbe huo umeelekezwa kwa wakazi wote wa Ulaya, ambamo kwa wakati huu kuna mwelekeo wa kutaka kutelekeza Ukristo kwa kishindo kikubwa. Marais wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki wa Ulaya, walitoa onyo hili wakati wa mkutano wao uliofanyika huko Monaco . Mwisho wa Mkutano huo, Maaskofu walimchagua Rais Mpya , chini ya Usimamizi wa Kardinali Angelo Bagnasco.
Maaskofu wamesema, pale dini inapotumiwa katika uhalisi wake , huwa na nguvu za kukuza vizuri ubinadamu na maendeleo shirikishi. Kwa mtazamo huo, Maaskofu wameonyesha matumaini yao kwamba, barani Ulaya, ambapo kwa wakati huu mna ishara nyingi za kuweka pembezoni majukumu ya Kikristo, kupitia vitendo vya kibaguzi, kwa fikira kwamba , malimwengu ndiyo yenye kuifanikisha jamii , hizi ni fikira potovu. Ni muhimu kwa jamii ya Ulaya kutambua maana na thamani halisi ya dini katika jamii na katika maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla..
Katika mkutano huu wa kwanza wa mwaka , Maaskofu pia walizungumzia dharura ya kupata jawabu kwa ongezeko la matukio mengi yanayoleta mateso makubwa kwa Wakristo, sehemu mbalimbali za dunia. Maaskofu wametoa tamko lao kali lenye kulaaani matukio yote yanayoathiri haki za binadamu na uhuru wake na hasa haki kwa dini. Maaskofu wamelaani dalili zozote zile zinazchochea moto wa vurugu na madhulumu yanayomotishwa na sababu za kidini wakisema huu ni unyanyasaji na ukiukwaji wa matumizi ya jina la Mungu.
Kwa maoni hayo Maaskofu wametoa ombi lao kwa setrikali zote duniani , zikatae katakata matumizi ya ghasia na dhuluma kama njia ya kueneza dini , kama ambavyo kwa mara nyingi Papa Francis, amelalamikia matumizi ya jina la Mungu , kufanya fujo na ukatili , akisema huku ni kukana haki za binadamu na Mungu pia . Wamesema , wao wakiwa Maaskofu katika mkutano huu wa Monaco, wakiongozwa na wasiwasi wanaouona kupitia kazi zao za kichungaji, wanatoa wito kwa wahusika na kuwaongoza watu , kiserikali au kimamlaka kitaifa au mataifa, , kufanya kazi ya ziada ili kuhakikisha heshima na uadilifu wa watu binafsi na jamii unarejeshwa kama ilivyokuwa katiak miaka yanyuma, na hasa kwa wale amba sasa wanaishi katika mazingira magumu zaidi.Ujum be wa Maaskofu hasa unaelekeza mawazo kwa Wakaristo wahamiaji na wale wanoteseka kwa sababu ya imani yao.
All the contents on this site are copyrighted ©. |