2016-10-11 14:41:00

Papa akemea vikali unafiki


Uhuru wa Mkristo hutoka kwa Yesu na si kutokana na utendaji wa mtu . Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza wakati akiongoza Ibada ya Misa, mapema  Jumanne hii,  katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican. Homilia yake ilitafakari kwa kina somo kutoka barua ya Mtume Paulo kwa Wagalatia na pia Injili ya siku ambamo Yesu anakemea unafiki wa mafarisayo, kujifanya kuwa watakatifu kumbe mioyo yao imejaa udhalimu na uovu.

 “Ninyi Mafarisayo , huosha kikombe na sahani kwa nje lakini ndani mmejaa udhalimu na uovu”. Yesu aliwaonya kwamba,  aliyetengenza nje  ni huyohuyo pia aliyetengeneza ndani pia. Na hivyo akawahimiza watoe kwa maskiini walivyo navyo na vingine vyote vitakuwa halali kwao.(LK.11;38-42)

Baba Mtakatifu aliyarejea maneno hayo makali ya Yesu kwa Mafarisayo, ambayo yaliyorudiwa mara kwa mara  katika Injili kwa Mafarisayo  kwamba ndani mwao mmejaa ukatili,  watu wasiokuwa wa haki na wala si huru. Na kwamba , walitajwa kwamba ni watumwa kwa sababu hakukubali haki itokayo kwa Mungu, haki iliyoletwa na  Yesu kwa binadamu wote.

Papa aliendelea kufafanua  juu ya uhuru wa ndani, uhuru wa kutenda mema  kwa siri, bila ya kujionyesha au kupaza sauti na kujitaagaza kama  tarumbeta , lakini ni kuifuta njia ya dini ya kweli, kimyakimya kwa utulivu, , kama Yesu  yalivyokuwa maisha ya Yesu, yaliyojaa  unyenyekevu,  na kujishusha .  Ni Yesu mwenyewe kama Mtume Paulo anavyoandika katika  barua yake kwa Wafilipi, kwamba unyenyekevu wa kweli ni njia pekee ya kuondokana na ubinafsi, ulafi, kiburi, ubatili, na katika kuyapenda ya kidunia. Yesu anakemea kufuata dini kwa sababu za kujionyesha  kumbe ndani  mteketezwa na uovu, kama yalivyo makaburi, kwa nje yanapendeza lakini ndani mmejaa uvundo wa mifupa na miili inayooza ya wafu. 

Baba Mtakatifu ametoa  mwaliko kwa wote kumwomba Bwana,  atusaidia kutembea katika njia yake ya  kweli,  na bila ya kuwa wanafiki. Kutenda mema katika hali ya  kimya kimya bila kudai malipo ikama shukurani kwa kuwa mema yote  tunayapokea kwa uhuru  ndani mwetu.  Ni yeye Bwana anayetupatia na kuudumisha uhuru huu kwa kila mmoja wetu. HIvyo basi na tumwombe Bwana  neema hii, Papa alimalizia.








All the contents on this site are copyrighted ©.