2016-10-03 08:58:00

Papa akamilisha ziara yake Georgia na Azerbaijan


Jumapili  majira ya saa 11 .15 za jioni kwa saa za Italia , ikiwa sawa na saa moja  na robo za Azerbaijan, , Baba Mtakatifu Francisko,  alikamilisha  ziara yake ya Kimataifa ya Kitume ya 16, ambamo ametembelea mataifa mawili , Georgia na Azeibajan. Ziara iliyo anzia  Georgia  Ijumaa iliyopita 30 Septemba. Kisha  Azerbaijan mapema Jumapili 02 Oktoba , ambako kati  ya matukio makuu ilikuwa ni kuongoza Ibada ya Misa katika Kanisa la Maria Mkingiwa dhambi ya Asili la mjini Bakù, mjini Mkuu wa Azerbaijan. Pia kukutana na viongozi wa kidini, Sheikh Mkuu wa Bakù na Rais wa Jumuiya ya Wayahudi katika eneo hilo. 

Nia kuu ya  Papa kwenda Azerbaijan , ilikuwa  kuwatia moyo ndugu zake katika Kristo, waendelee kuishikilia imani yao kwa uthabiti, licha ya kuwa kundi ndogo kati ya Waislamu wengim na pia kuhimiza ujumbe wa amani na umoja miongoni mwa watu wa mkoa huo, licha ya tofauti za kiitikadi na kidini.  Papa alitoa himizo hilo wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa la Maria Mkingiwa dhambi ya Asili lililko katikati ya Baku, Ibada iliyofuatiwa na  khafla ya chakula cha mchana na Wanashirika Wasaelsiani.

Taarifa ya mapokezi yaliyofanyika mapema Jumapili  asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kimataia wa Heydar wa  Bakù, zinaeleza kwamba, Papa alipokewa na Naibu wa kwanza wa Waziri Mkuu wa Azerbaijan ,  Mheshimiwa Yaqub Eyyubov na maofisa wengine wa serikali. Baadaye majira ya jioni Papa , alikwenda kukutana na Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan, Rais  Ilham Heydar, na na pia maofisa wengine wa kiserikali katika kituo cha  Heydar Aliyev.

Papa alikamilisha  ziara  yake kwa kufanya mazungumzo ya faragha na Sheikh wa Mkuu wa Kiislamu wa eneo la Caucasus katika Msikiti wa Heydar Aliyev, ikifuatiwa na mkutano mwingine wa faragha pia na Askofu wa Kanisa la Kiotodosi la Baku , na Rais wa jumuiya ya Wayahudi. Papa alitumia takribani  ya saa kumi, katika taifa hili la Azerbaijan kabla ya kuagwa na wenyeji wake wa Azerbaijan, katika uwanja wa ndege wa kimataifa,  Heydar Aliyev , majira ya saa moja na robo kwa saa za Azerbaijan. Na alitu akatika uwanja wa Kimaataifa wa Ciampino majira ya saa nne za usiku kwa saa za Roma.  

Hii ilikuwa ni ziara ya Kipapa ya 153 kwa Papa kwenda nje ya Italia katika nyakati hizi  sasa . Papa Yohane Paulo II , alitembelea Georgia mwaka 1999, na Azerbaijan mwaka 2002, kwa nia ya kutia shime jumuiya ndogo ya Wakristo katika mataifa hayo waendelee kumshuhudia Kristo Mfufuka kuwa ni Bwana Mkombozi wa Dunia na ni Bwana wa amani. 








All the contents on this site are copyrighted ©.