2016-10-01 16:42:00

Papa Francis aongoza Ibada ya Misa katika uwanja wa Tbilisi Georgia


(Vatican )Jumamosi hii tarehe Mosi  Oktoba 2016, ikiwa ni siku ya Pili ya ziara ya Kimataifa ya 16 ya  Baba Mtakatifu Francisko, nchini Georgia,  majira ya asubuhi,  aliongoza Ibada ya MIsa katika Uwanja wa Meskhi wa Mjini Tbilisi.

Katika homilia yake alitoa maneno ya faraja kwa jumuiya ndogo ndogo Katoliki za Georgia na mwaliko kwa waumini wote kuwa na upendo na umoja  kama ule wa watoto wadogo , ambao upendo wao humvutia Mungu.  Papa Francisko pia ameliwataja wanawake kuwa ni hazina kuu ya kutunza imani kwa taifa. 

Akimnukuu Mtakatifu Tereza wa Mtoto Yesu, ambaye sikukuu yake  imeadhmisha katika liturujia ya Jumamosi hii , Papa amesema kuwa wanawake wanaonekana kuwa na upendo mkubwa kwa Mungu kuliko wenzi wao wanaume.  Alieleza kwa kutazama kwa kina jinsi wamama na mabibi  wa Georgia , bila ya kuchoka hutetea na kurithisha njia ya imani, kwa watoto wao  kuliko wafanyavyo  wanaume. Alieleza kwa kutazama mfano wa maisha ya Mtakatifu Nino , anayetambuliwa kuwa mwenezaji wa kwanza wa Injili katika Karne ya nne..

Na kwamba kama mama achukuavyo matatizo na  uchovu wa watoto wake, ndivyo hata Mungu hubeba Yeye  Mwenyewe dhambi zetu na matatizo yetu kwa upendo wake  usiokuwa na mwisho kwa ajili yetu.

Papa aliendelea kuwafariji waTwatu wa  Georgia, akiwaalika kila mmoja wao aufungue  wazi mlango wa moyo  ili waweze kufarijiwa nae Yesu.  Na kwamba Mungu daima yu tayari kutufariji wakati wa shida na mahangaiko ya maisha. Yeye hutuweka huru dhidi ya uonvu na hutuletea amani ya kweli na kutuongezea furaha katika maisha . Lakini, hata hivyo  akaonya kwamba, ili mtu aweza kufaidika na hilio ni lazima kuuweka moyo wazi kwa Yesu, kwa  njia ya kusoma kila siku ya Injili yake , kuwa na sala kimya kimya katika ibada na kukiri imani na  kupokea Ekaristi.

Ameonya iwapo mlango wa moyo utabaki umefungwa,Yesu hawezi kuingia. Yesu atabaki nje akisubiri kukaribishwa ndani , wakati  huo ukiwa katika hali ya kusongwa na kina cha uchungu na upweke. Papa alieleza na kutaja kwa jinsi watu wengi wanavyoishi katika mateso na madhulumu na hali za wasiwasi kwa kuwa wako mbali na Yesu. Wako mbali na upendo wa Injili , wameyabeba maumivu yao wenyewe.

Na hivyo ni muhimu kusikiliza na kuushi mwaliko wa kumjongelea Yesu na kumkaribisha ndani ya roho na kuwa kama mtoto mdogo , kwa maana Mungu huvutiwa na upendo huu wa mtoto, na humpenda na kumfariji . huo ndiyo ujumbe wa Kanisa kwa watu wote leo hii , Papa alisisitiza.  








All the contents on this site are copyrighted ©.