2016-10-01 13:51:00

Papa akutana na Mkuu wa Kanisa la Upatriaki wa Georgia yote


Papa Francisko , siku ya Ijumaa majira ya jioni akiwa Tbilisi Georgia, alikutana na  Patriaki Ilia II , Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiotodosi la Upatriaki ya Georgia yote, wakiwepo pia wajumbe wa  Baraza la Sinodi Takatifu la Kanisa la Kiotodosi la Georgia. Katika hotuba yake Papa Francisko , alionyesha kutambua umuhimu wa ziara iliyofanywa na Patriaki Ilia mjini Roma mwaka 1980 , ambayo ilikuwa ni ziara ya kwanza kwa Patriaki wa Kanisa la Kiotodosi la Georgia kutembelea Vatican. Na pia ziara iliyofanywa na Papa Yohana Paulo II nchini Georgia , wakati wa Jubilee ya  Mwaka Mtakatifu wa  2000.

Hivyo katika mazingira ya kumbukumbu hii, hotuba ya Papa Francisko ililenga katika kile kinachounganisha makanisa haya mawili ambacho msingi wake umejengea juu ya Mahubiri ya Mtume Andrea kwa Kanisa la Kiotodosi na Mtakatifu Petro kwa Kanisa la Roma, ambayo ni ndugu wawili walioitwa na Yesu. Kwa mtazamo huo, Papa Francisko amemtaja Patriaki Ilia kuwa ni ndugu yake , na  aliomba wamruhusu Bwana Yesu  awaangalie upya na  kwa mara nyingine wapate mvuto kwa wito wake, unaowataka waache kila jambo linalowazuia kwenda kutangaza pamoja uwepo wa  Yesu Kristo Mfufuka , Bwana wa maisha.

Papa aliendeleea kuutaja upendo wa Kristo kuwa ndiyo msingi wa Umoja wa Wakristo, akisistiza juu ya upendo huu wa kweli wa Bwana kwamba , una nguvu ya kuwainua  kutoka dimbwi la utengano na kutenda kazi kwa pamoja. Kuwatoa katika hali ya kutoelewana ya nyuma ,kwa  sasa na hata kwa siku zijazo.Papa alieleza na kuonyesha kutambua kwamba , Watu wa Georgia, wameshuhudia  ukuu wa upendo huu karne kwa karne ,  upendo unaoongoza katika  "uzuri milele"  unaoonekana kuwa urithi wa utamaduni wa Georgia. Na aliomba wamepokee kama rafiki wa kweli wa Georgia na watu wake wapendwa, akiwataja kuwa ni watu  wapendwa wenye kuwa na ukarimu wa kipekee, wasiosahau mema waliyopokea yenye kuwaunganisha katika kutembea pamoja kwenye njia ya  umoja, njia ya maisha, wakiwa wamegubikwa katika matumaini  ingawa hapakosekani changamoto na  matatizo.

Papa Francisko  alihitimisha hotuba yake na kwa kuomba ushujaa wa kijasiri wa historia Georgia,  wa  Mtakatifu  George, uwawezeshe kutambua  jinsi ya kuushinda  uovu.  Papa aliomba maombezi yao , yaweze kuleta faraja kwa Wakristo wengine hata leo hii,   hasa wale wanaodhulumiwa na wanao kata tamaa , waweze kuimarisha ndani mwetu uvuvio adilifu  wa udugu ulioushikamana katika  umoja  kwa ajili ya kutangaza Injili ya amani.








All the contents on this site are copyrighted ©.