2016-09-29 16:50:00

Papa Francis amtunukia zawadi ya heshima Mama Janeth Mhella


Mwandishi wa habari  idhaa ya kiswahli wa Radio Vatican Mama Janeth Mhela Alhamis 29.10.2016. ametunikiwa zawadi ya heshima , medali ya  msalaba  kwa lugha ya kilatini “Pro Ecclesia et Pontifice”kwa  kwaajili ya shukrani katika  huduma  ya kutumikia  Radio ya Papa.

Mama Janeth Mhella wa idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican amekuwa mwafrika  wa kwanza kutunukiwa zawadi ya heshima  na Papa Francis , kwaajili ya utendaji mzuri wa kazi na huduma ya Kanisa.

Ametunikiwa zawadi kwa heshima na baba mtakatifu Francis  medali ya msalaba wa heshima na cheti kwa ajili ya kutambua  huduma nzuri aliyoifanya.

Zawadi hizo amezipokea kutoka mikononi mwa  Monsinyo Dario Edoardo Viganò, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya mawasiliano  wa Vatican kati ya watu wengine watano waliopata zawadi ya heshima  ya kitakatifu  katika sekretarieti ya mawasiliano.

Mwisho wa mwezi wa Octoba 2016 Janeth Mhella anastaafu kutoka katika Radio Vatican baada ya kufanya kazi kwa miaka 23.

Sr Angella Rwezaula.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.