2016-09-26 15:48:00

Ujumbe wa Papa kwa Makatekista: kamwe msichoke kumshuhudia Kristo Mfufuka


(Vatican) Kudumisha ukweli wa imani ya  Mkristo  kwamba Yesu Kristo ni Bwana,  aliyekufa na kufufuka, na  kamwe hatakufa tena , ni kiini  msingi katika imani ya Mkristo, anayotakiwa kuishuhudia  daima na popote, kushuhudia ukuu, utakatifu  na ushindi wake dhidi ya mauti. Kwa muhtasari , Papa Francisko, alieleza  katika homilía, aliyoitoa wakati wa Ibada ya Misa, mapema Jumapili iliyopita, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la MtakAtifu Petro  Vatican. Nia Kuu ya Ibada, ilikuwa  adhimisho la Jubilee Maalum ya Makatekista , katika mwaka Mtakatifu wa Huruma, kama ilivyopangwa ifanyike  Jumapili ya 26 ya Kipindi cha kaiwada katika Kalenda ya Liturujia ya Kanisa Katoliki.  

Baba Mtakatifu Francisko, alilitafakari fumbo la Pasaka, kiini cha imani ya Kikristo , akiitaja Ekaristi kuwa sawa na mapigo ya moyo yanayotoa uhai kwa kila jamb o, na hasa katika kutangaza fumbo la Pasaka , Mbiu Kuu ya kwanza kupigwa kwamba, Bwana Yesu  aliyekufa na kufufuka, yu hai hayumo tena kaburini. Papa aliendelea kueleza juu ya fumbo hili la Pasaka ambamo Yesu anayonyesha upendo wake usiokuwa na kipimo kwa watu wote, anayetolea maisha yake msalabani   kw aupendo mkuu, kwa ajili ya kumkoboa binadamu dhidi ya dhambi zake.  Papa alieleza na kuwahimiza Makatekista kushuhudia ukweli huu , Yesu alikufa msalabani , kuzikwa kaburi na kufufuka . Sasa yu hai,  yuko karibu nasi na anatusubiri kila siku. Papa alieleza kuwataka  Maktekista kuzingatia hilo kama jambo la lazima katika ushuhuda wao na mafundisho yao.   

Maelezo ya Papa yalilenga katika masomo ya siku na hasa Injili ya Jumapili  ambamo mlitolewa mfano wa mtu maskini Lazaro na mtu tajiri  akisema kwamba , , mfano huu unaolenga kutufundisha jinsi Bwana anavyowajali na kuwahudumia  watu kupitia sisi wenyewe,  na hasa  wale ambao wanapuuzwa katika maisha ya hapa duniani, na jinsi itakavyokuwa baada ya kifo chetu. Hivyo mfano huu wa Lazaro na Tajiri , unatupa fundisho la kutafakari dhamiri na wajibu wetu katika kupelekea  habari njema  kwa watu wengine na hasa kwa wale wanaohitaji zaidi, yaani maskini wa roho.

Baba Mtakatifu aliendelea kulenga katika  maadhamisho ya  Jubilee  ya Makatekista katika mwaka Mtakatifu wa Huruma na kuhoji iwapo walikuwa tayari kutimiza wajibu wa kupeleka habari njema ya wokovu kwa watu wote bila kujisikia wachovu. Na iwapo wanadumisha  ujumbe msingi wa imani  kwamba Bwana alifufuka na yu kati yetu.  Aliwaonya Makatekista kwamba, katika kazi zao zote,  hakuna jambo jingine lililo muhimu zaidi ya Kutangaza ushindi wa Kristo dhdi ya mauti.  Na kwamba, kila jambo linalo husishwa na ukweli huu msingi huzaa matunda mazuri na hasa  iwapo litazingatia kaulimbiu ya Pasaka. Na kwamba utendaji wowote unaotenganishwa na ukweli huu,  kwamba  Kristo  alikufa na kufufuka na sasa yu hai kati yetu ,  hupoteza  nguvu yake.

Kwa Maneno hayo, Papa alitoa  baraka zake kwa Makatekista wake kwa waume , akimtaka kila mmoja wao afanywe upya  kila  siku kwa furaha ya  kuwa mtangazaji wa mbiu ya Injili kwamba,  Yesu alikufa na kufufuka, sasa yu hai na anaishi kati yetu na  Yesu anampenda kila mmoja wetu.  Papa aliomba uwezo wa Kristo,  uwapatie wote ujasiri na nguvu za kuishi na kutangaza amri ya upendo na kuondokana na upofu  na huzuni za kidunia. Aliwaombea ili wawezeshwe  kuwaona maskini kama Lazaro, ambao Injili haikuwapuuza,  lakini daima huona umuhimu wao na hujifunua  wazi mbele ya watu wote. 








All the contents on this site are copyrighted ©.