2016-09-12 13:15:00

Dunia yakumbuka tukio la kigaidi la tarehe 11 Septemba


(Vatican Radio) Jumapili  dunia ilikumbuka tukio baya la kighaidi lililofanyika mjini New York Marekani  tarehe 11 Septemba 2011, lililodhuru maelfu ya watu  baada ya majengo mawili marefu ya marekani kuporomoshwa chini kwa shambulio la kigiadi karibia kwa wakati mmoja.  Mahali yalipokuwa majengo hayo pamebaki  uwanja wa wazi wa makumbusho unaojulikana kwa jina ” Ground Zero ”.

Baba Mtakatifu Francisko alipozuru Marekani mwaka jana Septemba 25 , 2015, alitembelea mahali hapo, na kutolea sala ya kuomba amani kwa dunia na kwa ajili ya  kuwakumbuka kafara wa tukio hili, lililo semekana kufanywa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda .

Baba Mtakatifu Septemba mwaka jana akiwa hapo, aliomba amani kutoka kwa Mungu akisema  ”Bwana shusha amani yako katika dunia hii yenye ghasia. Amani katika mioyo ya watu wote,  amani  kwa wanawake na wanaume, amani kati ya mataifa ya dunia hii.”

Na akitoa hotuba fupi mbele ya umati wa watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo, wakiwepo viongozi kutoka dini na mila mbalimbali za dunia, alipataja  mahali hapo kuwa ni mahali pa kutoa machozi , mahali pa kuwalilia kafara wote wa ugaidi, chuki na kisasi.

Hotuba hiyo ilisisitiza umuhimu tena kama lazima kujenga umoja uliosimikwa katika misingi ya wingi wa lugha , tamaduni na dini .  Papa aliwaaka  watu wote kujikatalia kila aina ya sumu na uharibifu unaoweza kuharibu mahusiano ya binadamu. Na kwamba ni lazima binadamu wote kushirikiana pamoja, kujenga familia moja ya binadamu licha ya utofauti wa kitamaduni na kiimani ni lazima kuwa na roho patanifu katika utofauti.  Na kwamba sote kwa pamoja tunatakiwa  kusema "hapana" kwa kila jaribio linalotaka kulazimisha watu kufanana. Ni lazima kusema "ndiyo" kwa utofauti wetu huku tukikumbatiana kwa upendo na kuheshimiana.

Alimalizia akiomba  amani duniani kote, amani katika dunia hii ambayo ni nyumbani kwa viumbe  wote, nyumbani kwa ajili ya wote. 








All the contents on this site are copyrighted ©.