2016-08-16 10:21:00

Papa :Sikukuu ya Maria Kupalizwa mbinguni, inatupa hamu pia ya kwenda mbinguni


Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu hii akiiadhimisha Sikukuu ya Maria kupalizwa mbinguni  roho na mwili , alisema inatupa hamu ya kutafakari kwa mara nyingi maisha ya Bikira Maria katika njia yake ya kuelekea Yerusalem ya mbinguni,  ambako alikutana na uso kwa uso na  Mungu Baba.  Papa alitoa maelezo hayo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana ,  mbele ya mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican.  Katika hotuba yake  ya kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, alitafakari Inijili ya Luka 1:39-56 ambayo inaeleza safari ya Maria kwenda kukutana na binamu yake Elizabeth.

Aya hizo,  Papa alisema zinatuongoza katika kutafakari kiroho, njia ya maisha ya Maria tangu katika mji wa Yerusalemu  na hatimaye kukutana  na uso wa Baba na kuuona tena uso wa  Mwana wake  Yesu.  Historia inaonyesha  katika maisha yake ya hapa Dunia, maisha ya  Maria yalijaa changamoto na uchungu mkali kama ilivyokuwa wakati wa mateso na kifo cha mwanae , katika mlima wa Karvari, aliko shiriki fumbo la  ukombozi ulioletwa na mwanae Yesu Kristo.  Baada ya kuikamilisha safari hiyo ,  Mama Maria , anafikia kilele cha mlima wa  maisha, ambako alivikwa mwanga wa  jua, na mwezi chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana 12,1), na  hivyo alikivuka vizingiti na kuingia katika  nchi ya mbinguni.

Papa alimtaja Mama  Maria,  kuwa mtu wa kwanza kumwamini Mwana wa Mungu, na ni wa kwanza kuchukuliwa juu mbinguni roho na mwili.  Alikuwa ni mtu wa kwanza kumpokea  Yesu  mikononi mwake  kama mtoto binadamu , na pia kuwa wa kwanza kukubaliwa kuingia ndani ya Ufalme wa milele wa Baba .  Bikira Maria, msichana mnyenyekevu  wa kawaida wa kijijini, anateuliwa na Bwana, kubeba tumboni mwake Neno la Mungu , kwa sababu yeye alikubali  kuiishi Injili, na hivyo anaruhusiwa na Mungu, kusimama  milele karibu na kiti cha enzi cha Mwana wake. Na hivyo Neno la Mungu linatimia kwamba ”Bwana atawashusha chini wenye nguvu kutoka kAtika viti vyao vya enzi na kuwakweza wanyenyekevu” .

Na hivyo kwa Maria kupalizwa mbinguni linakuwa ni fumbo kubwa katikA mtazamo wa maisha ya kila mmoja wetu kwa  siku  zijazo. Maria katika  ukweli wake , hutufuatilia sisi katika safari yetu ya maisha , tangu wakati wa kupata kubatizwa ambamo tunatoa ahadi ya kufungamana na Yesu  katika maisha , kama  Mama yake Maria, alivyoandamana na  Yesu siku zote.

 Papa alieleza na kuomba , katika sikukuu hii ya Mama Maria kupalizwa Mbinguni , na turudie ahadi yetu ya kutembea  katika njia inayoelekea katika dunia mpya  na mbingu mpya kama mashahidi wa  Kristo aliyefufukana kuyashinda  mauti , kumshinda nyule mwovu shetani.  Kwa hivyo, furaha ya msichana Mnyenyekevu wa  Galilaya, inaonekana katika wimbo wake mkuu ,uliomtukuza Mungu, na hivyo unakuwa ni wimbo wa wanadamu wote, wanaotafuta kuonana na  Bwana  juu mbinguni , wote wanaume na  wanawake ,  viumbe wanaoishi kwa unyenyekevu, ambão wamekaza macho yao juu mbinguni wakitamani pia kupaa pamoja na Mama Bikira Maria na kukutana na Bwana.

Papa alieleza na kuwakumbuka walio katika mateso hasa   wanawake waliozidiwa na  uzito wa mateso ya kimaisha na vurugu zinazofanywa dhidi yao. Wanawake walioingizwa katika utumwa kwa viburi cha wenye nguvu na mamlaka juu yao , wale wasichana wanaolazimishwa kufanya kazi za kinyama kama ukahaba, wanawake wanalazimika kutoa mwili na roho  zao kwa choyo cha watu dhalimu. Aliomba ili kwamba , kwa haraka  kwa ajili yao, ipatikane njia inayoweza kuwatoa katika dimbwi hilo la maisha na kupata  mwanzo wa maisha mapya ya  amani, haki na upendo, wakati wakisubiri mwanzo wa  maisha mapya , ambamo wanaweza kukumbatiwa  kwa unyenye kevu  na upendo wa kweli na huruma nyingi  yenye kuwaongoza hadi  katika upeo wa maisha ya  mbinguni.  Papa alisali na kujiweka katika uaminifu wa wa ulinzi wa Bikira Maria ,  Malkia wa mbinguni, akiomba  amani itawale katika njia za  njia  maisha yetu ,  hadi hapo tutakapo iona sura ya Mwanae Yesu ,  katika  furaha kamili ya maisha  ya  mbinguni.

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa alikabidhi kwa mara nyingine tena wasiwasi na huzuni za wakazi katika maeneo mengi ya dunia yanayo athiriwa na uwepo wa migogoro mbalimbali hasa mivutano ya kivita.  Alieleza hilo kwa kupeleka mawazo yake kwa wakazi wa eneo la Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambako hivi karibuni , kulitokea mfumko mpya wa ghasia zilizosababisha mauaji mapya.  Aliomba unyenyekevu wa Bikira Maria uguse   hisia zote za ufahamu na hamu ya maelewano!

Aidha aliwasalimu kwa upendo mkuu , vijana wote waliotoka Jimbo la Roma na kutoka mataifa mbalimbali , akitaja kwa namna ya  kipekee vijana kutoka  Villadose, na  jumuiya za waamini kutoka Credaro na wale wa Crosara, na kwa mahujaji na wageni waliofika kusali pamoja nae akiwataka  Sikukuu njema ya Maria Kupalizwa mbunguni , na pia kwa wote walio katika mapumziko ya wakati wa kiangazi , kwa wagonjwa na waliobaki ktika hali za upweke kutoka na hali zao za kiwmili na kwa wale wote waliyo yatoa sadaka maisha yao katika siku hizi za likizo kwa ajili ya kuwahudumia wahitaji , Papa alitoa salaam zake na kuomba pia wasimsahau katika sala zao kwa kuwa anahitaji maombezi yao. 








All the contents on this site are copyrighted ©.