2016-08-09 15:02:00

Salam za rambirambi za Papa kwa matukio ya kusikitisha


Jumatatu, tarehe 8 Agosti 2016, Papa Francisko mara baada ya kupta habari za maafa yaliyosababishwa na Kibunga kilichotwa Earl,  alituma salaam zake za rambirambi kwa njia ya telegram, kwa wahanga wa kibunga hicho kilichotokea eneo la  Amerika ya Kati.Maafa haya yamesaba bisha wau 13 kupoteza maisha na  hasara inayokadiriwa kufikia dola za Marekani milioni 50, katika katika Jamhuri ya Dominika na  Mexico watu 45 walipoteza maisha. 

Rambi rambi hizi za Papa ziltiwa saini na  kutumwa na Katibu wa Jimbo, Kardinali Pietro Parolin kwa Maaskofu wa Mexico na Domenican, Papa ameonyesha ukaribu wake na wote wanaofikwa na maafa haya akisema yupo pamoja nao kisala. 

Aidha kwa masikitiko makubwa,  Baba Mtakatifu Francisko amepeleka  salam zake za rambirambi kufuatia shambulio la kamikaze la Jumatatu  huko Quetta Pakistani, ambako mtu alijilipua kwa bomu akiwa hospitalini na kusababisha watu 74 kufariki na wengine karibia 200 kujeruhiwa.

Papa ameliita shambulio hili kuwa ni upunguani  na ukatili usiokuwa na maana yoyote isipokuwa kuangamiza maisha ya watu bure.

Katika telegram hiyo iliyotiwa saini na Katibu wa Jimbo la Papa, Kardinali Pietro Parolin, Papa Francisko, ameahidi kuwakumbuka kafara wa tukio hili katika sala zake , wazazi wa Marehemu na ndugu wa waathirika,na pia  mamlaka za utawala na  taifa zima. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.