2016-08-02 14:25:00

Michezo ni utamaduni wa kukutana!


Baba Mtakatifu Francisko katika nia zake za jumla kwa Mwezi Agosti anasema: “michezo ni utamaduni wa kukutana”. Kwa njia ya michezo inawezekana kabisa kujenga na kudumisha utamaduni wa watu kukutana, ili kukuza na kudumisha dunia inayosimikwa katika amani. Baba Mtakatifu anapenda kuwa na ndoto ya michezo ambayo kimsingi inajikita katika utu wa binadamu na kumwilishwa katika chombo cha udugu. Baba Mtakatifu anawauliza waamini na watu wote mapenzi mema, Je, wanapenda kuungana kwa pamoja ii kufanya mazoezi kwa njia ya nia hii ya Mwezi Agosti? Ili kweli michezo iweze kusaidia mchakato wa watu kukutana kidugu, ili hatimaye kujenga na kudumisha amani duniani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.