Jumamosi iliyopita 30 Julai , ilikuwa ni Siku ya Kimataifa ya Urafiki kati ya watu ikienda sambamba na siku ya Kimataifa dhidi ya usafirishaji haramu wa watu .
Siku ya Kimataifa ya Urafiki ilitangazwa mwaka 2011 na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa fikra kwamba, urafiki kati ya watu, nchi, tamaduni na watu binafsi, unaweza hamasisha juhudi za amani na kujenga madaraja kati ya jamii.
Azimio hilo namba A / RES / 65/275) linaweka mkazo hasa juu ya kuwashirikisha vijana, kama viongozi wa baadaye, katika shughuli za jamii, za tamaduni mbalimbali, tangu ngazi za chini hadi kimataifa na kukuza na kuheshimu tofauti zao. Siku pia nia ya kusaidia malengo na madhumuni ya Azimio na Mpango wa Utekelezaji juu ya Utamaduni wa Amani na kupinga Vurugu kwa Watoto wa Dunia.
Kwa adhimisho la mwaka huu 2016, Katibu Mkuu wa Moja wa Mataifa Bwana Ban Ki moon, ametoa ombi kwa kila mtu, kuungana katika roho ya pamoja ya mshikamano wa binadamu ili kuondokana na migogoro inayokabili jamii.
Ban Ki moon ameutaja Urafiki kuwa ndiyo furaha yenyewe ya maisha na ustawi wa mtu. Urafiki ni dhamana inayowezesha kila mtu kuchangia mageuzi makubwa ya haraka yanayotakiwa kufikia utulivu kudumu duniani. Na ameomba kupanua mikono katika urafiki na kujenga mahusiano ya kuaminiana, ili jamii iweze kufuma wavu wa usalama kwa ajili ya kuzishinda nguvu za makundi au majeshi yanayo jaribu kudhoofisha amani, usalama na maelewano ya kijamii.
Katibu Mkuu ana imani kwamba katika kuelewana na kufahamiana zaidi, pia hujenga moyo wa huruma kwa wengine na sana walio katika hali ngumu za maisha. Maelewano na umoja huzaa ulimwengu ulio bora zaidi, kwa kuwa huwezesha wote kushikamana katika umoja na hivyo kutendea kwa wema zaidi. Moyo wenye mapenzi ya kujenga urafiki na wengine hujinasua na itikadi za chuki na fitina na ukiukwaji wa haki za binadamu. Itikadi kama hizo kwa namna fulani huchukuliwa kama ni usaliti wa urithi wa ubinadamu na huweka hatarini ustawi wa wanadamu kwa wakati ujao.
Usaliti kama huo aliendelea kusema Bwana Ban, unaweza kushindwa tu kupitia njia ya umoja wenye kukuza na kutetea roho ya mshikamano na umoja wa binadamu katika kupambana na mzizi unaoleta changamoto katika maisha kama vile umaskini, vurugu na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Roho hii ya mshikamano, Katibu Mkuu alisema, ni wazi inaweza onekana katika njia nyingi, tangu katika mfumo wa ngazi ya chini wa urafiki binafsi hadi kaika ngazi ya kimataifa. Na alihitimisha ujumbe wake kwa ajili ya "Siku hii ya Kimataifa ya Urafiki” akitoa wito wa kutatua matatizo yaliyoko kwa kufanya mageuzi yenye kujenga uhusiano mzuri haraka iwezekanavyo, na kuyarutubisha maisha yetu wenyewe kwa amani na utulivu, kwa sasa na kwa ajili ya siku zijazo.
All the contents on this site are copyrighted ©. |