2016-08-01 14:31:00

Papa Francisko atuma salam za amani na matashi mema!


Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anarejea kutoka Poland kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016, Jumapili tarehe 31 Julai 2016 alituma salam za amani na matashi mema kwa viongozi wakuu wa Nchi ya Poland, Slovacchia, Slovenia, Croatia, Jamhuri ya Watu wa Czech na Italia. Anaishukuru kwa namna ya pekee familia ya Mungu nchini Poland kwa mapokezi na ukarimu wake na kwamba, anaendelea kuwaombea amani, ustawi na maendeleo kwa wote!

Baba Mtakatifu Francisko alipowasili kwenye anga la Italia alimtumia pia salam na matashi mema Rais Sergio Mattarella akimweleza kwamba, akiwa nchini Poland amekutana na vijana wa kizazi kipya ambao wako tayari kujenga madaraja, ustawi na maendeleo ya watu kwa kujikita katika tunu msingi za maisha ya Kikristo, mambo msingi yanayounda urithi wa kiroho wa Bara la Ulaya kama ilivyoshuhudiwa pia na wananchi wa Poland. Baba Mtakatifu anapenda kuwahakikishia wananchi wa Italia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake!

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.