2016-07-26 09:19:00

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Mkutano wa ”Laudato Si”Krakow Poland


Baba Mtakatifu Francisko kupitia Katibu wa Vatican , Kardinali Pietro Parolin, Jumatatu alipeleka ujumbe wake kwa mkutano unaozungumzia utuzaji wa mazingira duniani kama nyumbani kwa wote, mkutano unaendelea  huko Krakow Poland ambako vijana kutoka pande mbalimbali za dunia wiki hii wanakutana kwa ajili maadhimisho ya XXXI ya Siku ya Vijana ya Duniani.  Baba Mtakatifu Francisko atajiunga na vijana huko Krakow,  siku ya Jumatano hii 25 Julai ambako atakuwa huko hadi Jumapili tarehe 31 Julai. 

Katika ujumbe wake kwa mkutano wa Laudato Si, Papa Francisko amehimiza daima kuwa tayari  kusikiliza dalili za uharibifu na kifo kinacho andama binadamu katika safari yake ya maisha na  kuhamasisha taasisi kwamba mfumo wa uchumi usielekezwe peke yake katika matumizi ya maliasili bali uweze kuboresha kikamilifu utendaji wa  kila mtu na  maendeleo yake halisi .  Mkutano  huu wa "Laudato si" unaofanyika Poland kwa ajili ya Vijana, umeandaliwa kwa ushirikiano na Wizara za Mazingira za Italia na Poland,  Chuo Kikuu cha Papa Yohane Paulo II cha Krakow, Mfuko wa Msaada wa Yohana Paulo II, Shirika la Mwana wa Mfalme Albert II "wa Munich na kamati ya maandalizi ya Siku ya Vijana Suniani huko  Krakow.

Ni juhudi zinazolenga kuona uwajibikaji wa pamoja, kama ilivyoelezwa na Kardinali Stanislaw Dziwsz, Askofu Mkuu wa Krakow, kama msaada wa kutafakari  yanayofaa zaidi  kuzingatiwa kama wajibu kawaida katika kutunza viumbe kwa mujibu wa mpango wa Mungu  kama ilivyo katika asili yake.  Papa Francisko anavitaja viumbe wote kuwa ni zawadi ya kipekee kutoka kwa Mungu na hivyo inapaswa kutumiwa vyema  kwa manufaa ya wote. Na ili kuw ana fikira hiz, ni  lazima kuanza na mabadiliko katika maisha yetu ya kila siku kama kweli  tunataka kubadilisha maisha na kupunguza utamaduni w ulaji na taka, na kuwa na ufahamu kwamba, hata ishara ndogo zinaweza kuwa ni uhakika wa utendaji endelevu katika hatma ya familia ya binadamu. 

Mkutano huu ulianza Jumatatu katika Ukumb i Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jangellonica Jumatatu kwa ajili ya kufungua wiki la Maadhimisho ya XXXI ya Siku ya Vijana ya Dunia. 








All the contents on this site are copyrighted ©.