2016-07-16 15:26:00

Askofu Giuseppe Sciacca ateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Mahakama kuu


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Frans Daneels aliyekuwa Katibu mkuu wa Mahakama kuu ya Kanisa Katoliki na badala yake, amemteua Askofu Giuseppe Sciacca kuwa Katibu mkuu wa Mahakama kuu ya Kanisa Katoliki. Kabla ya uteuzi huo, Askofu Sciacca alikuwa ni Katibu mwambata Mahakama kuu ya Kanisa Katoliki.

Itakumbukwa kwamba, Askofu Sciacca alizaliwa tarehe 23 Februari 1955 huko Catania, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake, kunako tarehe 7 Oktoba 1978 akapewa Daraja Takatifu la Upadre. Kunako mwaka 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Gavana wa Mji wa Vatican na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu. Akawekwa wakfu kuwa Askofu hapo tarehe 8 Oktoba 2011.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.