2016-07-13 11:43:00

Kardinali Njue ni kati ya wajumbe wa Sekretarieti ya Mawasiliano


Baba Mtakatifu Francisko ameteuwa jopo la wajumbe wa Sekretarieti ya Mawasiliano mjini Vatican kati yao ni Kardinali: Béchara Boutros Raï, Patriaki wa Kanisa la Wamaroniti wa Antiokia (Lebanon); John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la  Nairobi (Kenya); Chibly Langlois, Askofu wa Les Cayes (Haiti); Charles Maung Bo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Yangon (Myanmar); Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa Makanisa ya Mashariki; Beniamino Stella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wakleri.

Wengine ni Askofu mkuu Diarmuid Martin, Jimbo kuu la Dublin (Irlanda); Gintaras Grušas,Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Vilnius (Lithuania); Marcello Semeraro, Askofu wa Jimbo Katoliki Albano (Italia); Stanislas Lalanne, Askofu wa Jimbo Katoliki la Pontoise (Ufaransa); Pierre Nguyên V_n Kham, Askofu wa Jimbo Katoliki My Tho (Vietnam); Ginés Ramón García Beltrán, Askofu wa Jimbo Katoliki la Guadix (Hispania); Nuno Brás da Silva Martins, Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Lisbon (Ureno).

Wajunbe wengine ni Dr. Kim Daniels, Mtaalam mshauri wa uhuru wa kidini kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki. Dr. Markus Schächter, Jaalim wa maadili katika vyombo vya mawasiliano ya Jamii, Chuo kikuu cha München (Ujerumani); Dr. Leticia Soberón Mainero,Mwanasaikojoa na mtaalam wa mawasiliano ya jamii; tayari aliwahi kuwa ni mtaalam mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii kwa ajili ya nchi za Mexico na Hispania.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.