2016-07-06 09:00:00

Kampeni ya amani kwa taifa la Syria

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa Caritas Internationalis  Dr.Michael Roy, amesema katika na  mahojiano na Gisotti, juu ya ujumbe wa Papa, kwanza alivieleza vita vya Syria vya miaka mitano kwamba, vinavyoendelea kuharibu taifa hilo,  na hivyo kuna umuhimu wa kuinua sauti zaidi na  kwa nguvu zaidi katika nia za kufanikisha amani Syria .

Na alitaja kwamba  ujumbe wa Papa kwa njia ya video, unalenga  kuimarisha kampeni ya Shirika la Caritas Internationalis  kwa ajili ya amani nchini Syria, na una umuhimu wa kipekee katika kupaza sauti zaidi , pamoja na mashirika mengine ya ubinadamu , yanayolilia amani kwa ajili ya Syria. Wote wka pamoja kuinua sauti kwamba, bado inawezekana kuwa na amani , bado kuna nguvu ya kupata ushindi dhidi ya  vita vilivyodumu sasa miaka mitano .

Katibu wa Caritas Internationalis ametaja vipengere vitatu muhimu katika hili akisema,  kwanza ni muhimu zaidi ya yote,  ni kuliweka jambo hili mbele ya uso wa Bwana, kuomba msaada wa Bwana kupitia ibada maombi na sala, kumlilia  Bwana ajalie amani Syria na dunia nzima. Amesema haiwezekani kuendelea na utengano huu , unaoonekana Mashariki ya kati.

Pili ametaja kuwa  mbele ya uso huu wa mateso , kunakosekana msaada wa kihali kwa maelfu ya watu si tu kwa wakimbizi lakini pia kwa wanaoendelea kubaki Syria. Mpaka sasa , Caritas Internationalis inazungumizia upatikana wa msaada wa kukidhi mahitaji ya watu kati ya milioni saba hadi nane. Hiki ni kipeo cha hali ya juu kinachokabili dunia.

Hatua ya tatu katika kampeni hii ni kuzitaka serikali za nchi zote duniani na hasa zinazohusika kwa namna moja au nyingine na vita hivi , kushinikiza usitishaji wa marubano na mapigano kati ya pande zinazohusika. Na Kampeni inaonya kwamba,  hatua hii isiachiwe tu Umoja wa Mataifa au umoja wa Ulaya , Lakini wote ni lazima kujihusisha.

Anamalizia maelezo yake kwa kusema kwamba, kwa ajili ya kutia nguvu kampeni hii , na pia hamu ya Wakristo wote kuona vita hii inamalizika, walihitaji neno la kuitia nguvu kutoka kwa Papa, na wamefurahi kwamba, Papa Francisko ametoa ujumbe wake wenye kuunga mkono kampeni hii na hivyo anakuwa ni  sehemu ya kampeni ya Caritas Internationalis. , Ujumbe wa umewatia shime watu  wote wenye mapenzi mema,  kuendelea kutenda kwa ujasiri zaidi  na zaidi kwa ajili ya kusitisha vita hii. Ujumbe wa Papa , ni ishara ya nguvu katika kusema kwa sauti kwamba bado inawezekana raia wa Syria  wakaishi kwa amani, wakiwa wamechanganyika kikabila, kidini na kiitikadi. Ujumbe wa Papa ni mwaliko kwa watu wote kushiriki kaTika kampeni hii ya Caritas Internationalis inayotoa ujumbe mpya kwa ajili ya ukomeshaji wa vita Syria. 

Na alitaja kwamba  ujumbe wa Papa kwa njia ya video, unalenga  kuimarisha Kampeni ya Shirika la Caritas Internationalis  kwa ajili ya amani nchini Syria, na una umuhimu wa kipekee katika kupaza sauti zaidi , pamoja na mashirika mengine ya ubinadamu , yanayolilia amani kwa ajili ya Syria. Wote wka pamoja kuinua sauti kwamba, bado inawezekana kuwa na amani , bado kuna nguvu ya kupata ushindi dhidi ya  vita vilivyodumu sasa miaka mitano .

Katibu wa Caritas Internationalis ametaja vipengere vitatu muhimu katika hili akisema,  kwanza ni muhimu zaidi ya yote,  ni kuliweka jambo hili mbele ya uso wa Bwana, kuomba msaada wa Bwana kupitia ibada maombi na sala, kumlilia  Bwana ajalie amani Syria na dunia nzima. Amesema haiwezekani kuendelea na utengano huu , unaoonekana Mashariki ya kati.

Pili ametaja kuwa  mbele ya uso huu wa mateso , kunakosekana msaada wa kihali kwa maelfu ya watu si tu kwa wakimbizi lakini pia kwa wanaoendelea kubaki Syria. Mpaka sasa , Caritas Internationalis inazungumizia upatikana wa msaada wa kukidhi mahitaji ya watu kati ya milioni saba hadi nane. Hiki ni kipeo cha hali ya juu kinachokabili dunia.

Hatua ya tatu katika kampeni hii ni kuzitaka serikali za nchi zote duniani na hasa zinazohusika kwa namna moja au nyingine na vita hivi , kushinikiza usitishaji wa marubano na mapigano kati ya pande zinazohusika. Na Kampeni inaonya kwamba,  hatua hii isiachiwe tu Umoja wa Mataifa au umoja wa Ulaya , Lakini wote ni lazima kujihusisha.

Anamalizia maelezo yake kwa kusema kwamba, kwa ajili ya kutia nguvu kampeni hii , na pia hamu ya Wakristo wote kuona vita hii inamalizika, walihitaji neno la kuitia nguvu kutoka kwa Papa, na wamefurahi kwamba, Papa Francisko ametoa ujumbe wake wenye kuunga mkono kampeni hii na hivyo anakuwa ni  sehemu ya kampeni ya Caritas Internationalis. , Ujumbe wa umewatia shime watu  wote wenye mapenzi mema,  kuendelea kutenda kwa ujasiri zaidi  na zaidi kwa ajili ya kusitisha vita hii. Ujumbe wa Papa , ni ishara ya nguvu katika kusema kwa sauti kwamba bado inawezekana raia wa Syria  wakaishi kwa amani, wakiwa wamechanganyika kikabila, kidini na kiitikadi. Ujumbe wa Papa ni mwaliko kwa watu wote kushiriki kaTika kampeni hii ya Caritas Internationalis inayotoa ujumbe mpya kwa ajili ya ukomeshaji wa vita Syria. 

All the contents on this site are copyrighted ©.