2016-07-02 16:23:00

Papa Francisko asikitishwa na vitendo vya kigaidi huko Dhaka!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican analaani kwa nguvu zote vitendo vya kigaidi ambavyo vimepelekea mateka 20 kuuwawa kikatili na watekanyara 6 pia kuuwawa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini Bangladesh. Baba Mtakatifu anasema vitendo hivi vya kigaidi ni kinyume kabisa cha mapenzi ya Mungu na ni ukatili mkubwa kwa binadamu!

Baba Mtakatifu anapenda kuziweka roho za marehemu waliouwawa huko Dhaka, Mji mkuu wa Bangladesh chini ya huruma ya Mungu pamoja na sala kwa wale waliojeruhiwa ili waweze kupona haraka. Baba Mtakatifu anapenda kuwatia faraja wale wote walioguswa na kutikiswa na shambulio hili la kigaidi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.