2016-06-25 15:51:00

Homilia ya Papa katika Uwanja wa Gyumri Armenia


Kumbukumbu, imani na huruma ni mambo msingi muhimu katika kumfuata Kristo. Ni mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko wakati akihubiri  katika Ibada aliyoiongoza mapema Jumamosi hii tarehe 25 Juni 2016, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kitume  nchini Armenia. Ibada iliyofanyika katika uwanja wa Vartanàs Gyumri.

Papa akiainisha liturujia ya Neno lililosomwa na historia ya maisha ya Ukristo Armenia , aya kutoka Kitabu cha Nabii Isaya “ Watayajenga upya magofu ya kale, watasimika miji iliyobomolewa hapo kwanza,  uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita..( Isaya 61: 4) amesema kwamba,  maneno ya nabii Isaya ni matukio halisi katika nchi ya Armenia. Na kwamba baada ya uharibifu wa kutisha wa tetemeko la ardhi,  wamekusanyika pamoja mahali hapo kumshukuru Mungu kwa yote  yaliyofanywa upya.

Papa alitazama kwa kina  zaidi, ujumbe wa Bwana katika liturujia ya Neno au kwa maneno mengine, ni wapi Mkristo anatakiwa kuyajenga maisha yake. Papa katika kujibu hoja hiyo, ametaja vipengere msingi na muhumu vinavyotakiwa kwa Mkristo  kuyajenga maisha yake juu yake. Navyo ni kumbukumbu, imani na matumaini. Ni kuwa watu wa kuyakumbuka matukio ya nyuma. Pili ni  kuwa watu wa imani na matumaini kwa siku za baadaye na tatu ni kuwa na moyo wa huruma kwa ajili ya wengine, kuwajali wengine. Kwa hiyo maisha ya Mkristo hayawezi tangamana na kumbukumbu , imani na huruma. Katika mambo hayo matatu Mkristo anatakiwa kuyajenga maisha  yake bila kuchoka, na kuwa tayari kufanya ukarabati mpya pale ufa unapojitokeza.   

Aliendelea kufafanua kwa kina , nguzo moja baada ya nyingine akianza na kumbukumbu  kwa yaliyopita akisema kwamba, neema yenye kutuwezesha kuyakumbuka matukio ya nyuma, hutuwezesha pia kukumbuka kile alichotufanyia Bwana katika maisha yetu( Luka 1:72 ) Bwana anasema hajawasahau waja wake, lakini anawakumbuka. Mungu amewateua kwa upendo wake, na husamehe wanapomkosea.   Papa alieleza na kumtaka kila mmoja  kukumbuka mambo makubwa aliyofanyiwa na Bwana katika maisha yake, matukio muhimu yenye kugusa moyo, yanayotakiwa kutunzwa kama hazina,  kiakili na kiroho pia.   Na pia ni muhimu kukumbuka yaliyofanywa na watu wengine wa kale kama hazina ya thamani.  Amefundisha kwamba, kwa kutunza kumbukumbu za kale  tunaweza tambua wazi  uwepo wa Mungu ,  katika maisha ya yetu na maisha ya kijamii, kwamba Mungu bado yu pamoja nasi. Papa alieleza hilo, kwa kuyaelekeza  mawazo katika kumbukumbu za  Manabii na watakatifu wa tangu kale na siku hizi , watu wanaoendelea kushuhudia uwepo wa Mungu katika nyakati zote.  Bwana huwakumbuka katika uaminifu wake wa Injili , matunda ya kwanza ya imani na wale wote walioshuhudia hata kwa gharama ya damu yao  kwamba Upendo wa Mungu una thamani kuliko maisha yenyewe (Zab 63: 4). Na hivyo ni vyema kufanya kukumbuka kwa moyo wa shukrani,  jinsi imani ya Kikristo ilivyoweza kuwa pumzi ya  watu na moyo wa kumbukumbu za kihistoria.

Aliendelea na  kipengere cha imani, akiitaja pia kuwa ni matumaini kwa ajili ya siku zijazo  na kama mwanga unaomulikia katika safari ya maisha . Katika hili ametahadharisha kwamba , kw abahati mbaya mara nyingi imani hupambana na hatari nyingi zinazotaka kuufifisha mwanga wake,  kwa vishawishi  na  majaribu mengi mbalimbali. Hatari zinazodhoofisha uthabiti wa imani, hasa katika matukio ya nyuma,yakifanywa yaonekana kama vile ni mambo ya  kizazi kingine, ni mambo yaliyopitwa na wakati , hatari za kuifanya imani kama kitabu kizuri lakini kinachohifadhiwa ndani ya maktaba na kusaulika humo. Papa anasisistiza  Imani haiwezi kufungiwa ndani , vinginevyo itapoteza  ladha, nguvu na uzuri wake katika maisha mazuri , yenye  uwazi na chanya kwa wote. Pia imani hii ni maisha ya kukutana na kutembea na Yesu siku zote.  Na hivyo imani ni  uzoefu wa maisha yenye kuandamana na huruma ya Mungu wakati wote. Imani  huzaliwa  kwa kukutana na Yesu, mwenye kutufanya wapya kiroho kila tunapokutana nae kwa moyo wa imani ya kweli.  Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa watu wote kila siku kutafuta kukutana na Yesu, si kwa kuhudhuria tu ibada au kusoma neno, lakini ni kumwilisha Neno la Mungu tunalolisoma na kimyakimya kuifungua mioyo yetu katika sala kwa Upendo wake usiokuwa na kipimo , na hivyo kuweza kukutana na Bwana kwa furaha kuu inayolishwa na huruma yake.  Tunaweza fanya vyema zaidi katika maisha yetu kwa kukutana na Bwana katika  hali zote, iwe katika furaha au katika hali za uchungu na kusikitisha kwa kuwa yeye hutupa faraja zinazogeuza yote kuwa na sura mpya ya amani. Kwake Bwana, yote katika  maisha hubadilika na kupatasura mpya inayotufanya kuwa  huru na kuwa na watu kweli na uwazi wenye kustajabisha  wengine.

Papa alimazia kwa kufafanua kipenge cha tatu ambayo ni huruma akisema huruma ni upendo, mwamba wa upendo tunaoupokea kutoka kwa Mungu na kuutoa kwa majirani zetu. Ni mtindo wa maisha ya mfuasi wa Yesu yaliyojengwa juu ya moyo wa huruma .  Katika maisha haya ya upendo kwa wengine, uso wa Kanisa hufanya upya na uzuri wake kuonekana zaidi na zaidi .  Upendo thabiti ni kadi ya utambulisho wa  Mkristo, anayotakiwa kutembea nayo kila mahali na nyakati  zote hata katika njia zenye kutaka kupotosha. Upendo kwa mtu mwingine ni utambulisho halisi  Mkristo , ili wengine wapate  kushuhudia kwamba huyu ni mwanafunzi wa Kristo(Yoh 13:35).  Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa Wakristo wote aksiema, sote tumeitwa zaidi ya  yote,  kujijenga katika njia za ushirika, na  bila kuchoka kujenga madaraja ya umoja na kufanya kazi pamoja  na kuondokana na migawanyiko inayotutengenisha.  Wafuasi wa Kristo daima wanatakiwa  kuwa  mfano wa jinsi ilivyo vyema  kushirikiana na mtu mwingine, kwa kuheshimiana na roho ya mazungumzo, wakiwa na uhakika kwmaba, inawezekana miongoni mwa wanafunzi wa Kristo  kama walivyofundisha pia Mapapa watangulzi wake.  

Papa alikamilisha homilia yake maneno ya Mtakatifu Gregory, akiomba  huruma ya Mungu na zawadi yake ya upendo usi ona mwisho yaani  Roho Mtakatifu, mlinzi wa nguvu, na mwombezi na mleta amani, tunayemwinulia sala na maombi yetu , aweze kuwapatia wote neema ya kusaidiana moja  kwa mwingine kwa upendo na hurumiana. Papa aliendelea kumwomba  Roho mwema, mfariji na mwenye huruma, ambaye yeye mwenyewe ni huruma, aturehemu sote .

Mwisho wa Ibada hii , Baba Mtakaifu Francisko alitoa shukurani zake za dhati kwa Catholicos Karekin II na Askofu Mkuu Minassian kwa maneno na baraka zao.  Na pia alitoa  shukurani kwa Patriaki Ghabroyan na Maaskofu na Mapadre na pia viongozi wa Serikali na wote walio wapokea na kuwakaribisha kwa moyo wazi na uchangamfu mkuu. Na hakusahau kuwataja walioka nchi jirani na hasa kutoka mkoa wa Giorgia. Na kwa namna ya kipekeleka salaam zake kwa  wote ambao kwa ukarimu wao na  upendo na wema ,  wanasaidia watu wahitaji wake kwa waume, na wahudumu katika  hospitali ya  Ashotsk, aliyofunguliwa  miaka ishirini na mitano iliyopita na inayojulikana kama "Hospital Papa", iliyoanzishwa kwa ukarimu wa Papa Yohana Paulo II, ambayo uwepo wake unaendelea kuonyesha  ukaribu wa Kanisa kwa  watu walio katika hali za  mateso. Papa ametaja hizi ni fadhila na matendo ya huruma ya Wakatoliki yanayofanywa na Masista wa Mama Maria asiyekuwa na doa na Wamisionari wa Huruma ya Mungu wa Mwenye Heri Mama Teresa wa Calcutta. Kwao wote aliwaombea msaada wa Mama Bikira Maria uandamane nao siku zote katika njia hii ya udugu na amani.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.