2016-06-24 17:22:00

Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Armenia


Baba Mtakatifu Francisko  majira ya jioni ametembelea Ikulu ya  Armenia ambako alipokewa na mwenyeji wake Rais Serzh Sargsyan, huku kukiwa pia na maofisa wengine wa ngazi ya juu serikali na mabalozi wanaowakilisha nchi zao Yerevan. Hotuba ya Rais Sargyyan kwa Papa na ugeni wote , ilianza kwa kutoa shukurani za dhati kwa ziara hii ya Papa Francisko, ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakiisubiri. Na kwa niaba yake mwenyewe na watu wa Armenia , wamemkaribisha kiongozi wa Kanisa la Ulimwengu , katika aridhi ya Armenia, taifa la kwanza kutangaza kuwa nchi ya Kikristo ambalo lilivumilia mateso kutokana na kung’ang’ania utambulisho na tunu za kikristo kwa kipindi chote.

Rais Serzh akiitaja ziara hii ya Papa kuwa ya kihistoria , alionyesha pia imani yake kwamba hiki ni kipindi cha baraka, furaha na amani kwa taifa la Armenia. Na kwamba uwepo wake Papa Francisko unawajaza na jotojoto la upendo na mshikamano majumbani mwao na mioyoni mwao.   Na kwanembo ya ziara Papa , kuonyesha heshima kwa Armenia kama  “ Taifa la Kwanza la Kikristo , na kuifanya ziara hii kama  muhujaji ,  unakuwa ni ushuhuda katika huduma yake Takatifu,   kwa ajili ya watu wa Armenia. Na pia inaoyesha kiungo cha Kipekee kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kitume la Armenia . Kwa ajili hiyo alimshukuru Papa Francisko. .

Kisha Rais Sargyasyan, ,alitazamisha katika historia ya Armenia , taifa lillilotembelea pia na Papa Yohane Paulo 11 miaka 15 iliyopita, wakati Armenia ikiadhimisha kupita kwa karne 17 za taifa hilo kutangazwa kuwa nchi ya Kikristo. Na ziara hii ya Papa Francisko inakuwa ni tukio jingine muhimu linaloadhimisha kupita kwa miaka 25 ya kurejeshwa upya uhuru wa Armenia . Sherehe inayofurahiwa na kila raia wa Armenia.  Rais aliendelea kukumbusha jinsi ambavyo historia ya Armenia kwa kipindi kizima za milenia watu wake wamepambana na hali ngumu , tangu mauaji ya halaiki na ugandamizaji wa mataifa ya nje , ubaguzi na kukataliwa. Lakini pamoja na yote hayo kama taifa hawakupoteza imani yao katika  ubinadamu , uvumilivu na mshikamano . Na kwamwe haikuwahi kupoteza imani yake na tunu zake na upendo asili , katika kutoa mkono wa msaada kwa watu wahitaji.

Aliendeela kutaja jinsi uamuzi wa watu wa Armenia kutangaza Ukristo kama dini halisi tangu mwaka 301 akisema kwa hakika ni tukio muhimu katika historia ya dunia , iliyokwenda zaidi ya kutoa ufafanuzi wa hatima ya watu Armenia  katika  Imani ya Kikristo na hivyo kuwa utambulisho wa watu wa Armenia katika historia yao na utamaduni wao uliowaongoza hadi karne ya 21 hadi nyakati hizi  na siku ya leo. Na kwamaba kwa Armenia,  Ukristo ni zaidi ya dini , kwa kuwa ni mfumo wa maisha  unaowasukuma katika kuwa na hamu zaidi na zaidi ya kuishi kwa amani na kushinda changamoto zote zinazotaka kuvuruga heshima yao.  








All the contents on this site are copyrighted ©.