2016-06-22 15:17:00

Papa : tuombe kuguswa na kutakaswa na Yesu


Baba Mtakatifu akiendelea na kutoa Katekezi kwa mahujaji na wageni, juu ya Mwaka Mtakatifu wa Huruma ya Mungu, Jumatano hii, amelenga katika tukio la Yesu kumponya mtu Mkoma kama ilivyoandikwa katika Injili ya Luka(5:12-14.) Papa amekumbusha kwa jinsi ugonjwa wa ukoma kwa wakati ule ulivyochukuliwa kama ni laani ya dhambi, na hivyo kisheria walikuwa hawatakiwa kuchaganyikana na wengine. Lakini kama Mtakatifu Luka  anavyoeleza, mkoma huyo  akiwa amehamasishwa na imani , hakuogopa kupita katikati ya makundi ya watu na kumwomba Yesu amtakase. Papa anasema , kama Mkoma huyo alivunja sheria basi Yesu pia alivunja sheria kwa kumgusa na kumtakasa maradhi yake.

Papa aliendelea kulizungumzia tukio hili akisema,  linatufundisha kutokuwa woga na wanafiki, katika kukutana na kuwagusa watu maskini na wahitaji wanaoishi miongoni mwetu.  Na kwamba kukutana hakuishii tu hapo , lakini ni kufanya kama Yesu alimwambia mgonjwa wa ukoma,  yeye mwenyewe kwenda  kujiwasilisha kwa Kuhani, kushuhudia na kutoa sadaka, kwa ajili ya kuponywa kwake. Kumbe tukio hili linatufundisha kwamba,  Yesu  humtakatifusha kila mdhambi anayetafuta kukutana nae na kuomba utakaso wake. Na baada ya kutakaswa,  kwa imani ya kweli,  huzaa matunda ya kushuhudia upendo na huruma ya Mungu.

Papa amesema, huu ni mwaliko unaotolewa na Yesu kwa kila mmoja wetu,  kusikia hitaji binafsi la kukutana na kuponywa na Yesu. Hivyo Papa anahimiza kama ilivyokuwa kwa mkoma yule, nasi pia na tumgeukie Yesu kwa imani tuombe kukutana na kutakaswa nae na kisha maisha yetu yaitakangze zawadi ya huruma na msamaha wake na kuzaliwa upya kiroho.

Mkoma huyo akijitambua kuwa ni mchafu , anaonyesha imani yake katika nguvu za Yesu na kusema ukitaka waweza niponya. Hii inaonyesha jinsi imani yake ilivyokuwa na nguvu iliyokishinda ,  kila kipingamizi cha sheria na  kutafuta kukutana na Yesu. Yeye alipiga kelele, Bwana ukitaka , waweza kuniponya.  Kumbe nasi tunaalikwa sote , kila mmoja kwa nafasi yake, , kumwendea Yesu na kumwomba utakaso wake. Na Yesu anamsikiliza kila mmoja, kama tunamwomba kwa  kujiamini.

Mafundisho ya Papa yaliendelea kutazama hali halisi za maisha yetu na kuhoji ni mara ngapi , sisi tunakutana na mtu maskini, watu wanaokabili na hali ngumu mbalimbali, lakini kwa hali yao,  tunajitenga mbali nao,  hatutaki kuwagusa kwa sababu tutaonekana kama wao au tutaambukizwa nao?  Papa anaonya, dhidi ya tabia ya woga na kujitenga mbali akisema, haiwasidii watu hao kwa sisi kuwa na ukarimu, na huruma ya kutoa fedha nyingi,  lakini  tukajiweka mbali nao. Tunatoa fedha, kwa kutupa katika kibakuli kilicho mbele yao, bila ya kuw ana hamu yakuzungumza nao na kuzijua shida zao kwa kina. Tunakwepa kuwashika au kuwagusa, tukisahau kwamba, wao ni  mwili mwili wa Kristo!

 Papa aliongeza, Yesu leo hii anatufundisha tusiwe na hofu au woga wa kuwa karibu na masikini na wagonjwa na waliotengwa kwa sababu za hali zao za kimwili. Tusiwe woga wa kukutana au kuongoza na watu wenye matatizo, kama wenye  tabia za ushoga, wahamiaji na wakimbizi waliotoka katika nchi zao kwa sababu za mateso ya vita na kutengwa. Hawa ni ndugu zetu katika Kristo.

Papa Francisco anasema ni muhimu kwetu kumpa nafasi  kila mmoja wao katika  maisha yetu. Ni muhimu kuwajali wote wanaotuijia na kuomba msaada wetu.  Aliendelea kukemea tabia za unafiki wa  kujiona sisi ni safi, akisema sote tunahitaji kupiga magoti mbele za Mungu na kuomba, "Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. Papa alieleza na kuomba kila mmoja kabla ya kwenda kulala usiku, na asema mara tatu kwa imani kamili,  Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa. 








All the contents on this site are copyrighted ©.