2016-06-22 12:00:00

Hali halisi ya maisha na utume wa Kanisa Katoliki nchini Armenia


Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Armenia kuanzia tarehe 24- 26 Juni 2016  inaongozwa na kauli mbiu “Hija kwa nchi ya kwanza ya Kikristo”. Ingawa imekuwa ni nchi ya kwanza kupokea dini ya Kikristo na kuifanya kuwa ni dini rasmi nchini humo, kumekuwepo na maendeleo hafifu katika shughuli za kichungaji pengine kutokana na changamoto za kihistoria na mauaji ya kimbari yaliyopelekea wananchi wengi wa Armenia kuikimbia nchi yao. Kanisa Katoliki nchini Armenia ina Jimbo moja linaloundwa na Parokia ishirini.

Waamini wa Kanisa Katoliki wanahudumiwa na Mapadre 21 wa Jimbo na Mapadre watawa 6. Kanisa lina Mashemasi wa kudumu 2 na Watawa walioweka nadhiri zao za daima ni 20. Kuna Majandokasisi 63 ambao wako bado kwenye Seminari ndogo na Waseminari wakuu ni 6 tu kutoka katika majimbo 20. Kanisa Katoliki linamiliki na kuendesha shule 1 ya msingi na shule 35 za Sekondari. Kanisa lina hospitali 1 na Zahanati 20, nyumba za wazee 5. Katika mazingira kama haya, Wakristo hawana budi kukuza mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayojikita katika huduma makini na ushuhuda wa upendo kwa Kristo na Kanisa lake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.