2016-06-21 15:17:00

Kardinali Pietro Parolin akamilisha ziara yake Ukraine


Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican Jumatatu tarehe 20 Juni 2016 alikamilisha ziara yake nchini Ukraine ambako alikwenda kama mjumbe wa Papa, kuonyesha mshikamano wa Kanisa la Ulimwengu kwa  Wakristo wa Ukraine,  hasa wahanga wa vita ya muda mrefu katika mkoa wa Mashariki nchini Ukraine. 

Kardinali akitoa salaam za Papa kwa Viongozi wakuu wa Kanisa, Mapadre , watawa na walei wake kwa waume, alimshukuru Mungu kwa  neema ya pekee aliyomjalia ya kukutana na waamini wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraine na Waotodosi, wakati wa adhimisho lao la Siku kuu ya Pentekoste. Na alishukuru kwamba, ameweza kuuishi utajiri wa Liturujia Takatifu ya Siku kuu hii usiokuwa na kipimo.  

Na kwamba, kwa maongozi ya Roho Mtakatifu,  amekabidhi  kazi aliyoifanya kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyemtuma kufikisha salaam za upendo na baraka za Papa kwa wahanga wa ghasia za vita, na kuwapa  msaada wa kihali kama ishara ya wa upendo wa Kanisa la ulimwengu. Kwa ajili yao, wanakumbuka huruma na upendo wa Mungu kwa maneno yenye kutia moyo, ambayo pia wameyasikia katika Liturujia ya Siku yanayosema “Ni wewe mwenye kutuonyesha Mkombozi Mkuu wa wale ambao wanakabiliwa dhuluma na huwamulikia wale wanaokaa katika giza na kivuli cha kifo". Hawatajiskia tena kutelekezwa au kusahaulika hata kwa  ndugu zao na dada katika ubinadamu".

Kardinali alimwomba Roho Mtakatifu awe Mpatanishi Mkuu wa kazi zote zinazolenga kujenga amani katika taifa hilo na katika dunia hii inayotafuta kujenga minara kwa ujasiri wa kibindamu kama ilivyokuwa wakati wa kujenga mnara wa Babeli, walikanganyikiwa kwa lugha. Kwa sasa katika adhimisho la Siku kuu ya Pentekoste, ina iwe fursa ya kujenga maelewano na umoja si kwa bidii zao za kibinadamu lakini  kwa unyenyekevu, na utambuzi wa kugeukia hekima na utukufu wa sayansi ya Mungu, wakiwa wamejawa na imani kwamba, hakuna linaloshindikana katika njia ya majadiliano. Na kwamba huu ni wakati wa kuinua sauti zao kwa wimbo wa usawa na kwa ajili ya wokovu wa roho. Ni muhimu kwao wote kuunganisha nguvu  zote kutoka kwa Roho huyu mwenye kuwapa  uelewa mpya na  wenye kufikisha mwisho  chuki na fitina zote, na kuwa ma matumaini makubwa mapya kwa watu wote wa taifa pendwa na Mungu la Ukraine.

Kardinali Parolin, alieleza na kusema , pale panapokuwa na kusambaa kwa  lugha za moto, hapo kanisa linatakiwa kuonyesha kwa nguvu umoja zaidi na zaidi na waumini wote katika Kristo, kuwa na  Roho wa umoja anayetafuta njia ya kujenga ushirikiano zaidi kwa msaada usiokoma wa Roho Mtakatifu, aliyemo ndani ya wale wanaomamini. Udugu unaotakiwa kuenezwa kwawote wanaoamni na wale ambao bado wanamtafuta Mungu kwa Moyo wa dhati.  

Na pia akashukuru kwamba, katika siku hizi chache alizokuwa nchini Ukraine, wameweza shirikishana kama wana wa Kanisa Katoliki la Kigriki na ndugu zao wa Kanisa la Mashariki na hivyo anatumaini roho hii iliyoonekana, kwa njia ya Roho Mtakatifu, wataweza kuendeleza upya, baraka za majadiliano, yaliyoanzishwa miaka kumi na tano iliyopita na Papa Yohane Paulo II, alipofanya hija katika taifa hili. Na kwa  maombezi  ya watu wa Mungu, wataweza barikiwa, na kufikia taji ya haki na kuponywa majeraha yao  kwa  mafuta ya huruma. 








All the contents on this site are copyrighted ©.