2016-06-21 14:46:00

Crete: Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kiotodosi


(Vatican Radio) Patriaki wa Kiekumene BartholomewI, Jumatatu ya wiki hii alifungua Mkutano wa Baraza  Kuu la Waotodosi, unao fanyika katika Kisiwa cha Crete Ugriki.

Taarifa zinasema, , maandalizi ya Mkutano huu wa utakaochukua karibia wiki nzima,  yamefanyika kwa zaidi ya miaka 50. Hata hivyo bado, unakabiliwa na changamoto ya kuwaweka  nje ya Mkutano , viongozi kadhaa wa Makanisa hayo. 

Patriaki Bartholomew I,katika hotuba yake ya ufunguzi, licha ya changamoto hiyo, amepongeza umuhimu wa uwepo wa mkutano kama huo, ambao pia unahudhuriwa na wageni waalikwa kutoka Makanisa mengine ya Kikristo. Miongoni mwa wawakilishi wa Makanisa mengine,waliokuwepo wakati wa ufunguzi wa Mkutano ni  pamoja na Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Kikristo, Kardinali Kurt Koch, aliyeongoza ujumbe kutoka Kiti Kitakatifu.  

Kardinali Koch, akichangia maoni yake, wakati huo wa ufunguzi, kati ya mengine, alitaja umuhimu wa Mkutano kama huo,  katika uimarishaji wa uhusiano kati ya Makanisa ya Kiotodosi na Makanisa mengine,  likiwemo Kanisa Katoliki. Maelezo ya Kardinali yalilenga katika maelezo yaliyotolewa na  Papa Francisco katika waraka wake wa Injili ya Furaha, ambamo anazungumzia zawadi za Kiroho kwa Wakatoliki,  wanazoweza kupokea kutoka makanisa mengine ya kikristo, hasa kutoka umoja wa kisinodi wa Kanisa la Kiotodosi.

Kardinali Kurt Koch ameonyesha matumaini yake kwamba, mada kuu zilizochaguliwa kuongoza majadiliano yajayo, ya Tume ya Kimataifa ya pamoja ya  Wakatoliki na Waotodosi, zitaweza zingatia umuhimu wa umoja wa kisinodi, kikao cha mwezi Septemba mwaka huu nchini Italia.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.