2016-06-18 16:22:00

Mh. Padre Valentine Kalumba ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Livingstone


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Raymond Mpezele wa Jimbo Katoliki Livingstone kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401 § 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Mheshimiwa Padre Valentine Kalumba, O.M.I, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Theresa na Makamu mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Livingstone.

Askofu mteule Kalumba alizaliwa tarehe 16 Januari 1967, huko Mufulira, Jimbo Katoliki la Ndola, Zambia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre na Kitawa tarehe 22 Oktoba 2005 akapewa Daraja Takatifu la Upadre. Tangu wakati huo amewahi kuwa Mchumi na Paroko usu wa Parokia ya Mt. Michael, Jimbo la Mongu, Zambia; Msimamizi wa Parokia ya Mt. Laurenti wa Brindis, Jimbo Katoliki Mongu, Paroko wa Parokia ya Mt. Michael, Leopold pamoja na kuwa Mkurugenzi wa Radio ya Liseli, huko Mongu. Baadaye alihamishiwa huko Burkina Faso. Kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2014 amekuwani Wakili wa Shirika la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, huko Zambia. Jimbo Katoliki Livingistone ni sehemu ya Jimbo kuu la Lusaka, Zambia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.








All the contents on this site are copyrighted ©.