2016-06-15 14:02:00

Waziri mkuu wa Uholanzi akutana na Papa mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko Jumatano asubuhi, tarehe 15 Juni 2016 amekutana na kuzungumza na Bwana Mark Rutte Waziri mkuu wa Uholanzi ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Baba Mtakatifu na mgeni wake wamezungumzia uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili na baadaye wakajikita zaidi katika masuala ya kimataifa kama vile changamoto ya wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji pamoja na kuangalia masuala mengine yenye umuhimu wa pekee kwa Jumuiya ya Kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.