2016-06-15 15:03:00

Askofu mkuu Luciano Russo ateuliwa kuwa Balozi Algeria na Tunisia


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Luciano Russo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Algeria na Tunisia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Luciano Russo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Rwanda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Russo alizaliwa tarehe 23 Juni 1963 huko Lusciano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 1 Oktoba 1988 akapewa Daraja takatifu la Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Aversa, nchini Italia.

Tarehe 27 Januani 2012, Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu hapo tarehe 14 Aprili 2012. Tarehe 16 Februari 2012 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda na tarehe 14 Juni 2016, Baba Mtakatifu Francisko amateuwa kuwa Balozi wa Vatican huko Algeria na Tunisia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.