2016-06-11 14:39:00

Papa atoa ombi :walemavu washirikishwe kikamilifu katika huduma za kanisa


Jumamosi 11.06.16 majira ya adhuhuri, Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya Walemavu, uliofadhiliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Italia kama sehemu ya maadhmisho ya Jubilei ya  miaka 25 , tangu Idara kwa ajili ya utoaji wa Katekesi kwa watu wenye ulemavu kuanzishwa katika ngazi ya kitaifa

 Hotuba ya Baba Mtakatifu, ambayo ilitolewa kimaandishi, kwanza ameshukuru Baraza la Maaskofu ltalia kwa hatua hiyo inayoonyesha kuwajali kwa wenye ulemavu katika huduma za kichungaji. Papa ametaja mambo mawili muhimu ya kuzingatiwa kwamba, kwanza ni kutoa mwamko katika elimu ya imani kwa mtu mwenye ulemavu na hasa wale walio na hali mbaya na pili ni kuwashirikisha walemavu katika huduma za kanisa, wakiwa kama  sehemu ya watendaji watendaji katika jumuiya anamoishi mlemavu.

Baba Mtakatifu alieleza na kurejea kama ilivyosemwa katika mkutano huo  kwamba si tu kufikiria kukutana na Yesu katika maisha ya kila siku lakini pia walemavu wana mengi ya  kuishuhudia imani yao kwa  wengine. Kuna mengi yaliyokwisha fanywa kwao kupitia huduma ya kichungaji kwa  walemavu; Na kwa sasa, kuna haja ya kusonga mbele na utendaji, kwa mfano,  kutambua zaidi  uwezo wao wa kitume na kimisionari, na na thamani ya uwepo wao, kama sehemu ya mwili wa kanisa. Ni muhimu kuwa na utambuzi kwamba,  katika udhaifu wao, mna hazina ya siri ambayo inaweza leta upya katika jamii  ya Kikristo.

Papa ameeleza na  kumshukuru Mungu, kwa Kanisa kuwajali walemavu katika hali zao mbalimbali, wote wenye ulemavu wa kimwili, kiakili na kihisia, na mtazamo wa jumla wa kuwapokea kama wanakanisa.  Hata hivyo, ameonya kwamba , bado jitihada zaidi zinatakiwa kufanyika kwa ajili ya  uwepo utendaji wa kweli na ushiriki kamili wa mlemavu unaoonyesha uwepo wake kutambuliwa na  kukubalika kwa mtazamo kwamba watu wote ni sawa mbele uso wa Mungu , hakuna anayebaguliwa au kutengwa.

Hotuba ya Papa ameendelea kutaja huduma ya Masakramenti kwa walemavu kama zawadi ya Mungu na pia ushiriki wao katika Ibada za Kiluturujia akiitaka jumuiya ya kikristo kufanya kazi ili kwamba kila mbatizwa  anaishi na  Kristo kupitia utii na uaminifu katika ahadi kwa sakramenti.

Papa ameonya pia kwamba, ni muhimu kujali ushiriki wa watu wenye ulemavu wakati wa Ibada za kiliturujia kwa mfano wanaoweza kusimama au kutembea pia wapewe nafasi za kutoa mchango wao, kama kuiba au kupeleka mapaji.  Kwa mlemavu utendaji huu inakuwa ni ishara inayonyesha amepokewa ndani ya kanisa kama mmoja wa wanakanisa. Papa amekemea jambo lolote lenye kuwa na mtazamo wa kubagua walemavu.  

Hotuba imeonyesha matumaini ya Papa katika maadhimisho haya ya miaka 25 ya idara Katekesi kwa walemavu, kwamba umekuwa ni wakati wa kutafakari zaidi, jinsi gani wanaweza ongeza mwamko zaidi, katika huduma zaidi kwa watu maskini na wahitaji kama walemavu. Amesema ni lazima kusonga mbele kwa uvumilivu na ameomba msaada wa Mama Yetu Maria kinara cha Uvumilivu. 








All the contents on this site are copyrighted ©.