2016-06-10 15:26:00

Papa akutana na Ujumbe kutoka Usharika wa Reformed Churches


Ijumaa hii  Juni 10, 2016, ujumbe kutoka Usharika wa Reformed Churches”duniani, ukiongozwa na Rais wa Usharika huo Mchungaji Jerry Pillay na Katibu Mkuu Mchungaji Chris Ferguson, umepokewa na Papa Francisko mjini Vatican na kuwa na mazungumzo ya pamoja yaliyolenga kuimarisha   zaidi uhusiano kati ya Makanisa.

Papa akizungumza na ujumbe huo, kati ya mengine ameutaja  ugeni huo, kuwa ni hatua moja mbele  katika juhudi za kiekumene, na pia ni baraka na matumaini katika njia ya kutembea pamoja kwenye jitihada zinazotafuta kuwa na  umoja kamili  kwa mujibu wa Sala ya Bwana "ili wote ulionipa wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja”(Yn 17:21 ).

Papa katika hotuba yake kwa  ujumbe huu wa  Makanisa ya Reformed Churches, imesisitiza kama jambo la kidharura , kukuza uwezo wa kiekumeni, katika kazi za   uinjilishaji na huduma ya kiroho,  sadaka ya uponyaji na ukombozi unaopatikana katika kanisa la Kristo.

Papa Francisko amekubusha pia kupita kwa ipindi cha zaidi ya miaka kumi tangu ujumbe kutoka ushariki  Reformed Churches, ulipofanya ziara yake Vatican na kupokewa na Mstaafu Benedict XVI, umoja unaoonyesha mafanikio kuelekea ujenzi wa umoja wa Wakristo, na hivyo inakuwa ni  chanzo cha faraja kwa wengi wanaotembea katika njia ya ekumeni.

Papa ameendelea kumshukuru Mungu kwa undugu uliopo , kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyoandika, si matokeo ya moyo wa hisani au  roho ya kifamilia isiyoeleweka , lakini inatokana na utambuzi wa mzizi  wa umoja unaochipushwa na Ubatizo mmoja na wajibu wa kumtukuza Mungu katika kazi yake (cf. Ut Unum Sint, 42). Aliendelea kusema, katika ushirika huu wa kiroho, Wakatoliki na madhehebu mengine ya Kikristo , wanajitahidi kuwa  pamoja, katika njia hii y aumoja kwa ajili ya kufanikisha kazi za  Bwana.

Kwa mtazamo huo, Papa amesisitiza kama jambo la kidharura, kufanikisha majadiliano ya kiteolojia, yanayolenga kuondoa utamaduni wa  kutoelewana katika  mafundisho kati ya Wakristo, pia uwezekano wa  kukuza zaidi ushirikiano kwa ajili ya uinjilishaji na huduma.

Baba Mtakatifu Francisko alieleza na kurudia kutoa shukurani zake za dhati kwa ziara yao  na majitoleo yao katika huduma kwa Injili. Na pia alionyesha tumaini lake kwamba kukutana kwao , inekuwa ni  ishara madhubuti katika  safari ya  pamoja kuelekea umoja kamili. Anasema kuwa huenda tukio hili, likawatia moyo zaidi  wajumbe wote wa tume inayohusika na marekebisho yanayoendelea kufanywa kwa pamoja kwa ajili ya kufanikisha matumaini na faraja zaidi kwa waamini wa Kanisa.  

Ujumbe kutoka ushariki wa Maknisa ya Reformed Churrches uliomtembelea Papa Francisko ni pamoja na Rais wa Ushariki  Mchungaji. Jerry Pillay, Katibu wa Ushariki  Mchungaji Chris Ferguson, akiwepo pia Mchungaji Dora Arce Valentin, Katibu mtendaji kwa ajili ya haki;  na Dk. Aruna Gnanadason, mshauri kwa teolojia na  Gabriela Mulder, rais wa Ushariki wa Presbyterian na Amerika ya Kusini na Caribbean; Mchungaji Eugene Bernardini, msimamizi wa Kanisa la Valdese, na  Phil Tanis, ambaye ni Katibu Mtendaji kwa ajili ya mawasiliano katika Ushirika huo. 








All the contents on this site are copyrighted ©.