2016-06-05 13:26:00

Bikira Maria waongoze watoto wako katika utakatifu, haki na amani!


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu wapya wawili, mashuhuda wa Fumbo la Pasaka, amewashukuru waamini wote walioshiriki kwa wingi katika maadhimisho haya. Kwa nama ya pekee ameushukuru ujumbe kutoka Poland uliokuwa chini ya uongozi wa Rais Andrzej Duda pamoja na ujumbe kutoka Uswiss uliokuwa chini ya Bi Alice Bah Kuhnke, Waziri wa Utamaduni nchini Uswiss.

Baba Mtakatifu ameyaombea mataifa haya mawili baraka, ulinzi na tunza kutoka kwa watakatifu hawa wapya waliotangazwa na Mama Kanisa, Jumapili tarehe 5 Juni 2016.  Baba Mtakatifu pia amewakumbuka waamini na mahujaji kutoka ndani na nje ya Italia waliofika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kushuhudia matendo makuu ya Mungu kwa waja wake. Baadaye kidogo, Baba Mtakatifu ameongoza Sala ya Malaika wa Bwana, ili Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa aweze kuwaongoza na kuwasindikiza waamini katika hija ya utakatifu na mchakato wa ujenzi wa haki na amani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.