2016-05-28 09:02:00

Papa Francisko : Kiini cha Imani ya Mkristo ni Yesu aliyemo katika Ekaristi


Alhamis majira ya jioni  katika Kanisa Kuu la Laterani, Papa Francisko aliongoza Ibada ya MisaTakatifu  iliyofuatiwa na Maandamano ya Ekaristi takatifu hadi kwenye Kanisa  Kuu la Mama Maria Mkuu katikati ya Jiji la Roma,  kwa ajili ya maadhimisho ya Sikukuu ya Ekaristi Takatifu, Sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo,  itakayofanyika katika makanisa mengi siku ya Jumapili ijayo kutokana na sababu za kichungaji, ili kuwawezesha waamini wengi kushiriki katika tafakari ya Fumbo kuu la maisha na utume wa Kanisa.  

Katika homilia yake, Papa Francisko,  alitafakari Ekaristi kama mzizi Mkuu wa  nguvu za Kikristo, tangu mwanzo wa Ukristo na katika maisha yote ya Kanisa  kama inavyodhirishwa na maisha ya watakatifu, watu mashuhuri katika kanisa waliyoyatolea maisha yao kwa upendo,  katika  kuhudumia mwengine , majitoleo ya maisha yasiokuwa na kujibakiza , kuleta mkate mezani kwa  wale wasiokuwa navyo wake kwa waume, kama baba au mama wa familia aafanyavyo kila siku kwa familia yake.  Kwa namna hio Papa aliwakumbuka Watakatifu , wazazi na Wakristo wengine  wengi  wanaorarua maisha yao vipandevipande katika  kuhudumia wengine.

Alihoji , leo hii ni mama   na baba  wangapi,  ambao kila siku wanachapa kazi kwa bidii ili waweze kuyakimu maisha ya kila siku, kuweka mkate kila siku juu ya meza majumbani mwao  au wale  ambao mioyo yao imepodeka kwa ajili ya kufanikisha watoto wao si  kukua tu lakini kukua vizuri. Na ni Wakristo wagapi, kama raia wema, wameyatolea maisha yao kwa ajili ya kutetea hadhi utu wa mtu kwa binadamu wote, hasa maskini, wanyonge na wale wanaobaguliw? Wakristo hao  wapi hupata  nguvu za kufanya hivyo?

 Papa alihoji na kutoa jibu kwamba ni katika Ekaristi, Mkate uliomegwa kwa ajili ya wote ndimo mna  makazi ya upendo wa Bwana Mfufuka ,ambao hata leo hii unamegwa ,  wenye kuhamasisha moyo kuwapenda wengine na kuwa  watu wa huruma. Katika Ekaristi mna uwezo wa  Bwana Mfufuko,  ambaye leo huu pia,  anaumega mkate na kurudia kusema “ fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu “.  Papa aliongeza kusema , hata maandamano ya Ekaristi yatakayofanyika baada ya Misa , ni kitendo kinachoonyesha kutoa chakula hiki kwa watu leo hii, ni kuumega mkate wa maisha kama ishara ya upendo wa Kristo kwa ajili ya jiji la Roma na dunia kwa ujumla.

Baada ya Ibada ya Misa , kulifanyika  maandamano ya  Ekaristi kutoka Kanisa Kuu la Yohana wa Laterano hadi katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu . Maandamano yaliyokusanyika pamoja makundi ya waamini kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo la Roma , mashirika na taasisi za Watawa,  mashirika ya hisani na mshikamano wa kidugu  na watu wote kwa ujumla . Maandamano yanayolega kuwashuhudia wale wasioamaini bado kwamba kiini cha fumbo la Imani ya Kikristo ni kwamba kweli Yesu yumo kweli katika maumbile ya Mkate na Mvino wakati wa maadhmisho ya Liturujia ya Ekaristi. 








All the contents on this site are copyrighted ©.