2016-05-27 14:49:00

Papa: awataka wafuasi wa Don Orione kuhudumia umma bila kuchoka


Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Mkutano Mkuu wa Shirika la Don Orione, umehimiza  wanashirika kudumu katika mwendo wa pamoja wa wafuasi wa Kristo , kwa kuwa kanisa zima limeitwa kutembea na Kristo katika njia zote za dunia kwa ajili ya kukutana na ubindamu leo hii,  kama hitaji muhimu zaidi na kama alivyoandika mwanzilishi wa Shirika hilo "kutoka katika Mkate na Divai mna faraja za Mungu wa imani" (Barua II, 463).

Papa ameeleza hilo na kutoa mwaliko kwa Wanashirika wa Don Orione, kuyamwilisha  maneno haya ya muasisi wa shirika na kuyaishi mafundisho yake, ambayo wameyaweka kama dira ya kuongoza Mkutano wao Mkuu na pia katika Utumishi wao kwa Kristo na maskini .  Na kwamba,hiyo inakuwa ni njia yao ya daima yenye kuwaunganisha na pia ni vipimo viwil katika maisha yao iwe  maisha binafsi na au utume wa usharika. Aliendelea kuwakumbusha kwamba, wameitwa katika maisha wakfu na Mungu kwa ajili ya kukaa pamoja na Yesu na kuwatumikia maskini na waliotengwa kijamii. Katika hao wanautumikia ndimo mna mwili wa Kristo unawataka kukua katika muungano Nae,  daima wakitakiwa kuitunza  imani, na kuwa macho ili  isije geuka kuwa itakadi na huduma isiyo isiyokuwa ya hisani. 

Papa aliwataka kuwa Wasamaria wema, na zaidi ya yote kuwawezesha watu wengi zaidi na zaidi kuifikia barabara ya kutembea pamoja na Yesu mkombozi wa dunia , na mwenye kuwapa furaha kamili ya kweli katika maisha yao .Alihimiza ni  kuwakutanisha wote na Yesu, mwenye kuwaweka huru dhidi ya dhambi ,mwenye  kuondoa huzuni zinazotokana na mambo ya kidunia, utupu na upweke wa kutengwa katika jamii.Na kwamba Yesu Kristo, mwenye uwezo wa kuyageuza maisha i daima huzaliwa  upya  kwa furaha  ndani ya mioyo ya wanaomridhia. 

Aidha ametahadharisha kwamba, utangazaji huu wa  Injili, hasa katika siku zetu, unahitaji kuwa na  upendo kwa Bwana,na   majitoleo kwa ajili yake.  Na hivyo akawasihi wasijifungue sehemu moja bali watoke na kwenda mbali wanakohitajika. Ma huduma yao kwa Kanisa itakuwa fanisi zaidi,iwapo wanajibidisha kwanza kabisa kuponya dhamira zao binafsi kwa Kristo na malezi yao ya kiroho, ili ushuhuda wao uwe wa  kweli wenye kuonyesha  uzuri wamaisha yaliyo wekwa wakfu, maisha mema ya "watumishi wa Kristo na maskini wa kiroho ,  wakiwa kama mfano kwa vijana.  Papa alieleza na kutoa msamiati wa maneno kwamba, "Maisha huleta maisha", na maisha ya bora ya kidini yenye furaha,  huweza hamasisha miito mpya.

Papa alikamilisha hotuba yake kwa kuwaweka wanashirika wote chini ya Ulinzi wa Bikra Maria ,wanaye mheshimu kama Mama  wa Kudra ya Mungu.  Na aliwasihi pia wasimsahau katika sala na maombi yao. Mwisho akawapa  baraka zake za Kitume kwao wenyewe na wale wanaowahudumia  wazee na wagonjwa, na wale wanaoshirikishana nao karama za Taasisi yao.








All the contents on this site are copyrighted ©.