2016-05-24 14:53:00

Papa Mstaafu : hakuna kilichofichwa katika Siri ya tatu ya Fatima


Papa mstaafu Benedikto XVI amesema, Siri ya Tatu ya Fatima ilitolewa kikamilifu, mwaka 2000, na hakuna kilichofichwa au kubakizwa .  Papa Mstaafu alieleza katika tamko lake lililochapishwa  katika makala ya siku ya Jumamosi na Ofisi ya habari ya Vatican, kuhusu "Siri ya Tatu ya Fatima." Hivi karibuni, zimetolewa  makala kadhaa juu ya siri ya tatu , ikiwemo maelezo yaliyotolewa  na Profesa Ingo Dollinger ambaye ameeleza kuwa  baada ya uchapishaji wa Siri ya Tatu ya Fatima (uliofanyika  Juni 2000), Kardinali Joseph Ratzinger , alimdokeza kwamba,  uchapishaji wa siri ya tatu haukuwa kamili.

Papa mstaafu Benedict XVI, amekanusha maneno hayo akisema , kamwe hajawahi  kufanya mazungumzo na  Profesa Dollinger  juu ya Siri za Fatima. Na kwamba maelezo yaliyotolewa na Profesa Dollinger juu ya jambo 'ni uzushi  usiokuwa na ukweli wowote. Papa Mstaafu anathibitisha kwa mara nyingine kwamba , Yaliyokuwa yameandikwa katika siri ya Tatu yote yalichapishwa kikamilifu kama ilivyokuwa. 

Siri Tatu za Fatima,  zilitolewa kwa watoto watatu wa Ureno wakati Bikira Maria alipowatokea watoto hao kwa mara sita kati ya Mei na Oktoba 1917. Siri mbili zilitolewa mapema mwaka 1943 kwa ombi la Askofu Jose Alves Correia da Silva wa Leiria kwa ajili ya kuchapisha kitabu kipya juu ya Jancita. Siri ya Tatu ilibaki kuwa ya mtoto aliyebaki hai,  ambaye alijiunga katika utawa  na kujulikana kwa jina la  Sr. Lúcia de Yesu Rosa Santos.  Kunako mwaka 1943 , Sr Lucia kwa shinikizo la Askofu aliiandika siri hiyo kwa mkono wake na kuweka maandishi hayo ndani ya bahasha akisema isifunguliwe hadi mwaka 1960. Bahasha iliyobaki imefungwa hadi mwaka 2000, wakati Papa Yohana Paulo 11 alipofungua bahasha hiyo na siri kutangazwa hadharani bila uficho.

Kwa mujibu wa ufafanuzi waVatican juu ya siri hizo, siri mbili zilizotangazwa awali zilitabiri juu ya Vita Kuu mbili za Dunia, na siri ya tatu ilitabiri shambulio dhidi ya Papa Yohana Paulo II , lililofanyika mwaka 1981.    








All the contents on this site are copyrighted ©.