2016-05-18 15:46:00

Kesi ya Vatileaks II yasikilizwa tena Vatican


 Kile kinachoitwa kesi ya Vatileaks namba mbili, mwanzoni wa wiki hii, ilisikilizwa tena na mahakama ya Vaticani. Taarifa imetolewa kwamba, Jopo la Wanasheria Jumatatu na Jumanne lilisikiliza maelezo,  jinsi nyaraka nyeti mbalimbali za siri za Vatican zilivyoweza kuvujishwa nje kwa waandishi wa habari wa Italia mwaka jana 2015.

Aidha Jumatatu  mahakama iliendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa Washitakiwa  Mons. Lucio Angel Vallejo Balda, na  Francesca Immacolata Chaouqui na Nicola Maio. Katika kikao hiki washitakiwa wengine , ambao ni Waandishi wa habari  Emiliano Fittipaldi na Gianluigi Nuzzi hawakuwepo  mahakamani badala yake waliwakilishwa na wanasheria wao.

Watu wengine wawili, Mario Benotti na Paulo Mondani, waliotakiwa kuwepo kwa ajili ya  kutoa ushahidi wao ,nao  hawakuonekana  mahakamani.  Na hivyo kutokana na kutokuwepo  kwao,  pande zote mbili. Mawakili wa utetezi wa washitakiwa na washitaki walikubaliana kufuta ushahidi wao.

Hata hivyo , ushahidi zaidi ulitolewa na mashahidi wengine wanne, ambao ni  Fabbio  Schiaffi kutoka Idara ya Uchumi , Lucia Eccoli, afisa katika kitengo cha afya Vatican, Mons. Vittorio Trani, Padre wa gerezani Roma Regina Caeli na Kamisheni wa kikundi cha polisi kinachotoa ulinzi Vatican 








All the contents on this site are copyrighted ©.