Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi akiendelea kutoa Katekesi kwa ajili ya Jubilee ya Mwaka Mtakatifu wa Huruma, aliitafakari huruma yenyewe, ambayo ni kati ya vipaji saba vya Roho Mtakatifu. Alisema kwamba, mara tunaposikia neno hili, tunapata hisia ya unyenyekefu fulani wa kidini au huba ndani mwetu wenye mvuto wa mkubwa wa kuwaelekea wale wanahitaji upendo zaidi au kuhurumiwa.
Papa aliendelea kuitaja huruma kuwa ni kielelezo cha upendo wa Mungu kwa viumbe wake kama ambavyo mara nyingi tunavyosoma katika Injili. Tunaiona huruma ya Yesu kwa watu wengi waliokuwa katika hali ya mateso, wagonjwa, wenye mapepo, maskini na wanaoonewa , Yesu anajali mahitaji yao na kutoa jibu kwa huruma na upendo . Walimgeukia Yesu wakiomba huruma yake “ Bwana Nirehemu” (taz 10.47-48; Mt 15,22; 17,15)”. Yesu aliwatazama kwa huruma nao walipata faraja ya uwepo wake. Yesu aliwahimiza wamwamini Yeye na Neno lake , na alifanya miujiza ya uponyaji.
Kwa maelezo hayo Papa alitoa mwaliko kwa wote akisema kuwa sote tunatakiwa kumuiga Bwana wa huruma katika kusikiliza kilio cha wale wanaomlilia kutokana na kutofautiana kwetu au wale waliotengwa kwa udhaifu wao. Sote tunatakiwa kukujali mahitaji ya ndugu zetu walio katika matatizo na mateso iwe kiwili au kiroho. Papa alikamilisha katekesi yake akiomba msaada wa Bikira Maria, Mama wa huruma, Mfano wa mtu mwenye huruma, atuwezeshe kupata neema ya kuuishi Jubilee hii ya mwaka wa Huruma kwa kupata ukomavu zaidi katika huruma na upendo kwa wote kwa kuiiga huruma isiyokuwa na kifani ya mwana wake Yesu Kristo.
Baada ya Katekesi yake , Papa alisalimia kw akutaja makundi mbalimbali ya watu waliofika kumsikiliza. Kati yao walikuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mama Asiyekuwa na Ndoa, Pia Jumuiya ya Kipapa ya Mtakatifu Josaphat ya Ukraina, na washiriki wa kozi ya majiundo ya wakufunzi katika Chuo Kikuu Salesian. Pia Wanachama wa Chianti, wakiongozwa na Askofu Giovannetti., Shirikisho Katoliki kwa ajili ya ufadhil na wanachama Unitalsim na mahujaji wengi waliotoka Ufilipino na Uingereza na pande mbalimbali za dunia. Kwao wote Papa Frncisko ameonyesha matumaini yake kwamba, Jubilee ya huruma, pamoja na kupita katika Mlango Mtakatifu, inatoa fursa ya kufikisha kwa ndugu zetu huruma ya Mungu Baba, kwa wale wote wenye kuhitaji faraja katika shida zao.
Pia aliwasalimu vijana, wagonjwa na Maarusi wapya. Na aliwakumbusha kwmaba, Jumamosi hii ni sikukuu ya Mtakatifu Matthias, mtume wa mwisho kujiunga katika kundi la mitume kumi na wawili. Alisema nguvu yake ya kiroho, inawataka wapendwa vijana, hasa wanafunzi katiak Chuo cha Moyo Mtakatifu, na Chuo cha Paul VI cha hapa Roma, kuwa thabiti katika imani yao katika kutelekeza kazi za Bwana Mfufuka . Papa aliomba msaada wa Bwana uwagemeza katika huduma yao kwa wapendwa wagonjwa, katika nyakati za shida; na kujituma kwao kwenye utume wa kimisionari. Na aliwageukia wanadoa wapya akiwataka wakumbuke daima kwamba , upendo wao ni msingi katiika kuiunganisha familia.
All the contents on this site are copyrighted ©. |