2016-05-09 15:43:00

Ni wajibu wa wabatizwa wote kumtangaza Kristo kila mahali.


Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili  akisali sala ya Malkia wa Mbingu,Jumapili ya saba ya kipindi cha Pasaka, alihimiza Wakristo kumhubiri Kristo, kila mahali duniani bila woga. Himizo hilo alilitoa  mbele ya maelfu ya mahujaji na wageni  waliokusanyika  katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , Jumapili hii ambayo pia Mama Kanisa alikuwa akiadhimisha Sikukuu ya Kupaa Rabbi, na Siku ya Mama wote .

Akitoa hotuba fupi juu ya siku kuu  ya Kupaa Rabbi , Papa alisema, "awali kabla ya kuwaacha marafiki zake , Yesu alifanya rejea katika kifo na ufufuko wake , akisema ninyi ni mashahidi wangu. Na kumbe Yesu anawataja mitume wake waliokuwa mashahidi wakati wa mateso kifo na ufufuko wake pia wanakuwa mashahidi wake wakati wa kupaaa kwake Kristo"

Baba Mtakatifu aliendelea kusema, "Kwa kweli, baada ya kuona Bwana wao anapaaa mbinguni,  wafuasi walirudi mjini, wakishuhudia kwa furaha na guvu zote  kama mashahidi, walivyomwona Yesu akipaa mbinguni. Kwa furaha walitangaza  hilo kwa kwa kila mtu, na juu ya  maisha mapya yanayoletwa na Kristo Mfufuka,na  katika jina lake, walihubiri katika mataifa yote,  toba na msamaha wa dhambi.

Baba Mtakatifu aliendelea kusema, walikuwa mashahidi si kwa maneno tu lakini pia kwa matendo katika maisha ya  kila siku.Na hivyo Papa akatoa wito kwa wabatizwa wote wa Kristo akisema, ni kutoa ushuhuda  kila siku, kama inavyotangazwa na Makanisa kila Jumapili na kuendelea kwa wiki nzima, katika nyumba zetu, ofisi zetu, shule zetu, kukusanywa kwetu maeneo na kumbi za burudani, hospitali zetu, magereza, na nyumba kwa ajili ya wazee, katika maeneo inaishi  wahamiaji, nje na ndani ya miji. Ni lazima kupeleka ushuhuda  huu kila wiki kwamba  Yesu kapaa mbinguni , lakini yu pamoja nasi.  Kristo ni hai!

 Pia Papa wakati huo wa sala la Malkia wa Mbingu , aliwakumbuka  Wamama wote duniani,  kwa kuwa pia ilikuwa ni Siku ya Dunia ya kuwaenzi wamama wote, wenye watoto hata wasiojaliwa watoto.  Alisema" katika siku hii, kwa heshima na taadhima , tunawaenzi kwa upendo mkuu, wamama wote walio kati yetu na hata waliotutangulia mbele ya Uso wa Bwana. Kwao  wote tunawakabidhi kwa Mama Maria Mama wa Yesu".  Kwa ajili yao  wote Papa aliwashukuru  kwa  kuipokea dhamana hii ya kuwa mama waliyopewa na Mungu na kwa ajili yao  alisali ya Salaam Maria. 








All the contents on this site are copyrighted ©.