Mjumbe wa Mungu huwa na mbinu za kuwafika watu maskini na kuwaweka huru dhidi ya matatizo yao, kwa kuwa amejawa na Roho Mtakatifu, mwanga na upepo wa nguvu wenye kutoa nguvu katika dhamira ya uinjilishaji. Ni ujumbe wa Papa Francisko kwa Kundi la Mapadre wa Shirika la Wamercedari waliomtembelea siku ya Jumatatu, mjini Vatican, kama sehemu ya Mkutano wao Mkuu wa nwaka na adhimisho la miaka kutimia miaka mia nane ya Shirika.
Katika hotuba yake fupi kwa Mapadri hao alionya dhidi ya majigambo kwa sifa nzuri za nyuma, bila ya kuwa na juhudi mpya zinazoendana na sura halisi ya nyakati hizi ambamo mnahitajika zaidi kuwa na njia mpya ya kutembeana katika njia ya karama , kufanikisaha haki, ukarabati wa makosa yaliyofanyika , na kujipa moyo na kuwa na msukumo mpya wa kufanya hivyo katika maisha ya kileo.
Aidha Papa alikitazama kipindi hiki cha miaka mia nane ya Shirika na kusema kwa hakika ni mingi . Kwa ajili hiyo, Papa Francisco atongoza Ibada ya Misa kwa kushirikiana na kundi la Mapadre hao wapatao 50 wanaoshiriki katika Mkutano wao Mkuu na baadaye atawapokea katika Ukumbi wa Makardinali ulioko katika jengo la Kitume ndani ya Vatican. Mkutano Mkuu wa Shirika unaogozwa na Mada Mbiu: Wamercede: “kumbukumbu na unabii katika mazingira uhuru”.
Akionyesha kufurahia jina la Mkutano Mkuu, Papa Francisko, alisema kweli ni jambo jema kukumbuka kazi kubwa iliyofanyika katika miaka hii mia nane ya Shirika. Lakini kumbukumbu hiyo isitie ujinga wa kubaki kujivunia tu yaliyofanyika katika kipindi hicho, bali ni lazima yaliyofanyika yatumike kama kioo katika utendaji wa wazi na ufahamu wa kujua wapi panahitajika kurekebishwa au kuongezewaa nguvu au palipo sahaulika, lakini bila ya kwenda nje ya mipaka ya shirika na hasa katika kukabiliana na changamoto zinazogandamiza ubinadamu. Ni muhimu kwa shirika kutafuta mbinu mpya za maisha ya shirika kwa ajili ya kuendelea kukabiliana changangamo za leo na kuvumbua majibu yenye huduma kwa mahitaji halisi ya dunia na ya Kanisa, na wakati huohuo, kubaki aminifu katika urithi wa kudumu uliachwa na wahenga waanzilishi wa Shirikaa, urithi unaopaswa kutunzwa kama lulu kuu ya shirika
Aidha Papa aliwaambia kwamba, ujuzi wao katika kidini ni zawadi na uwajibikaji mkuu wenye thamani sana. Hata hivyo, Papa aliasa juhudi si zao binafsi, lakini inatokana na kutegemea huruma ya Mungu daima ambayo ni nguvu na msaada kwa kila mmoja. Alisistiza umakini na uvumilivu katika sala na huduma ya hai ndani na nje ya shirika. Ni kwa roho hiyo tu , kama unavyonena utangulizi wa kitabu chao cha Mwongozo” Inawezekana kuzungumzia hali hali unabii, vinginevyo hatuwezi. Papa aliongeza akisema, huu ni mwaliko kwa wale walioipokea zawadi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuwatumikia watu.
Na kwamba "Nabii anajua anakotakiwa kwenda vitongoji, kuwakaribia watu na kuwaweka huru dhidi ya mizigo yao inayowalemea”. Na kinachomsukumu kufanya hivyo ni Roho Mtakatifu anayevuvia mwanga wa njia ya kutembea na kuwasukuma mbele katika utendaji wao wenye kuhimiza kutembea katika nyayo za watangulizi wao, Wahenga wao walioweza kubaki katika maishaya dhiki kama mateka na maskini, na watu waliotengwa katika jamii, kwa nia ya kuwafariji watu wanaokabiliwa na hali ngumu ya maisha kama hayo., wakichangia katika maisha ya kila siku, siku moja baada ya nyingine, hali ya uvumilivu na ukimya wa maishayaliyo huru na ukarimu, kwa manufaa ya wengine. Papa alieleza na kukukumbusha juu ya utume wao wa kuwakomboa maskini wa maskini kwa kufungamana nao na kuwatangazia habari njema hasa katika mwaka huu wa Huruma ili wote waweze kupeleka ujumbe huu.
Alihimiza , Ni kuwafikia wale wanaoteswa kwa sababu ya imani yao na wafungwa, waathirika wa biashara haramu, vijana mashuleni, na wote wale wanaosubiri matendo ya huruma ya waamini katika Parokia , na wale wote waliokabidhiwa kwao na Kanisa.
All the contents on this site are copyrighted ©. |