2016-05-02 07:36:00

Mh. Padre Mandla Jwara ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Ingwawuma!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Mandla Siegfried Jwara kuwa ni Askofu wa Jimbo la kitume la Ingwawuma, nchini Afrika ya Kusini. Askofu mteule alizaliwa tarehe 1 Februari 1957 Jimboni Mariannhill. Baada ya masomo na majiundo yake katika elimu dunia, tarehe 1 Februari 1981 akajiunga na Shirika la Wamissionari wa Mariannhill.

Baada ya malezi ya kitawa, kunako mwaka 1982 akaweka nadhiri zake za kwanza na hatimaye nadhiri za daima kunako mwa 1986. Baada ya majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 14 Februari 1987. Katika maisha na utume wake kama Padre, amewahi kuwa: Wakili Paroko kati ya mwaka 1987 hadi mwaka 1992. Kati ya Mwaka 1992 – 1993 alikwenda nchini Uingereza kwa masomo ya juu katika masuala ya maendeleo ya binadamu, uongozi, malezi na ujenzi wa Jumuiya. Kunako mwaka 1993 – 1998 alikuwa ni mlezi wa Wanovisi, Gombera na Mshauri wa Kanda. Kunako mwaka 1998 hadi mwaka 2002 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Kanda ya Mariannhill, nchini Afrika ya Kusini. Kati ya Mwaka 2002 hadi mwaka 2004 alikuwa ni mshauri Makao makuu ya Shirika mjini Roma. Mwaka 2005 hadi mwaka 2006 alikuwa ni Paroko na mshauri wa Shirika kikanda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.