2016-04-26 14:38:00

Askofu mkuu Francisco Padilla ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican Falme za Kiarabu


Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Bahrein na kwenye Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.  Itakumbukwa kwamba, kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Francisco Padilla alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania na baadaye kuteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kuwait na mjumbe wa kitume kwenye Kisiwa cha Kiarabu.

Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla alizaliwa kunako tarehe 17 Septemba 1953 Jijini Cebu, Ufilippini. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 21 Oktoba 1976. Tarehe 1 Aprili 2006 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Papia New Guinea na Visiwa vya Solomon. Tarehe 23 Mei 2006 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. Tarehe 10 Novemba 2011 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.