2016-04-18 09:19:00

Papa asema Ziara yake Lesvos : ishara ya Upendo na mshikamano wa Kanisa


 Baba Mtakatifu Francisko Jumapili akihutubia kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu, aliirejea safari yake fupi ya Jumamosi,  katika kisiwa cha Lesvos Ugiriki, akitaja madhumuni yake kwamba, alikwenda kuonyesha na  kuimairisha mshikamano wa Kanisa kwa wakimbizi na watu Greek. Na alionyesha kufurahia kukutana pamoja kwa upendo na kama ndugu na Patriaki wa Kiekumene  Bartholomeo, na Askofu Mkuu Jerome II wa Athens na Ugiriki yote  na hivyo kuwa ishara hai ya umoja wa wanafunzi  wa Bwana  mmoja Yesu Kristo.

Papa Francisko iliianza hotuba  yake mbele ya mahujaji wa wageni waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu kwa kutoa shukurani kwa  wote walioongozana naye  kupitia sala wakati wa safari hii. Na pia alikumbuka  yaliyojiri katika moja ya kambi za wakimbizi alizotembelea ambako Yeye Papa na wenzake waliweza kukutana na Wakimbizi zaidi ya 300 kutoka Afghanistan, Syria, Afrika Kaskazini na maeneo mengine ya dunia. Papa alionyesha kujali kwamba wengi wa wakimbizi hao ni watoto . watoto ambao baadhi yao wameshuhudia mauaji ya wazazi wao  au wenzao. Papa alisema, maelezo ya wakimbizi hao yanahuzunisha.  Alirejea  kisa cha Kijana wa Kiislamu aliyekuwa na watoto wake wawili ambaye mke wake Mkristo aliuawa na maghaidi wa Kiislamu kwa kuwa alikataa  kukana imani yake kwa Kristo. Papa amemtaja mama huyo kuwa ni Shahidi mfia dini.

Ziara hii ya Papa ya muda mfupi katika kisiwa cha  Lesbos, imeweza toa angalisho makini katika  hatma ya maelfu ya wahamiaji na wakimbizi  wanaovuka Bahari ya Mediterranean kwa lengo la kuingia Ulaya  kutafuta maisha mapya .

Aidha wakati huo wa sala ya Malaika wa Bwana , umati  ulikaa kimya kwa muda wa dakika chake wakati Papa alipowakumbuka kafara wa tetemeko baya ya aridhi lililosababisha  makumi ya watu kupoteza maisha huko Ecuador na pia huko Ujapan  Alhamisi iliyopita. Papa alitoa mwaliko wa kuwakumbuka kafara wa maafa haya asilia katika sala , kuomba msaada na huruma ya Mungu kwa waathirika wote , na wote walioguswa waweze pata nguvu na faraja za kudumu katika kumtegemea Mungu.  Aliitaja nguvu ya Imani , inayopatikana daima kwa Yesu Kristo, Mchungaji mwema, ambayo inayoadhimishwa katika kila Jumapili ya Nne ya Pasaka , kama Injili inayosema : Ninayatolea maisha yangu kwa ajili ya wanakondoo wangu na hakuna atayeweza kuwapokonya kutoka katika mkono wangu,

Papa aliomba maneno hayo ya Injili yaweze kuwa msaada katika kumfuata Kristo na katika kuifuta daima sauti ya Mchungaji mwema . Na kwamba si kuisikiliza sauti kinafiki , bali kwa utambuzi kamili na kutoa jibu  la kumfuata kwa unyenyekevu kwa  maneno na matendo kama wafuasi wake. Alisema inahusu kusikiliza si kwa masikio ya kimwili lakini masikio ya kiroho.

Kwa namna hiyo , Papa alitasema hakuna sababu za kuwa na hofia  maisha, kwa kuwa anayeyapoteza maisha kwa ajili ya Kristo huyaokoa. Upendo wa Yesu kwa wanafunzi wake hauna kipimo.  Aliwakumbusha Waamini kuwa macho kwamba, mwovu  shetani,  adui mkubwa wa Mungu na viumbe wake , hufanya kila hila ya kutaka kupokonya  waamini zawadi ya maisha ya milele waliyopewa na Mungu. Hata hivyo, Mwovu shetani hawezi kufanya kitu, kama hatutamfungulia milango ya mioyo yetu, kwa kufuata vishawishi vyake katika kutenda maovu.  Mwisho Papa alitoa salam zake kwa wote , akiikumbuka  maadhimisho ya Jumapili hii kama Jumapili ya kuombea Miito . Aliwataka vijana wote wa kike na kiume kumwomba Bwana awasaidie kutambua wito wao kimaisha si tu katika wito wa kuwa mapadre au watawa, lakini pia wito wao kama wafuasi wa Kristo. Na pia alionyesha ukaribu wake na familia nyingi zinazoishi katika hali za wasiwasi na maisha magumu kutokana na maatatizo ya ukosefu wa ajira.  Alionyesha matumaini yake kwamba, utendaji wowote ule utazingatia heshima na utu wa bindamu.  








All the contents on this site are copyrighted ©.