Watalaam wa maradhi ya akili, wameionya dunia kwamba, magonjwa ya akili ni kati sababu zinazoongoza katika kusababisha uwepo wa ulemavu unaoathiri mamilioni ya watu duniani,ikiwemo migogoro ya kibindamu. Hivyo huduma na tiba kwa wenye matatizo ya akili si suala la hiari au kama anasa lakini ni muhimu kupewa kipaumbele. Wataalam walieleza wakati wa mkutano wa Benk ya Dunia na Shirika la Afya Duniani uliofanyika wiki hii Washington Marekani. Mkutano pia ulifahamishwa kwamba idadi ya watu walioathirika na maafa yanayosababishwa na binadamu, imeongezeka mara mbili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita na idadi ya watu kuhama makazi yao kuwa ni zaidi ya milioni 60 ikiwa ni juu zaidi tangu wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia .
Shirika la Afya la Dunia( WHO) linakadiria maradhi ya akili, ikiwemo mfadhaiko, wasiwasi na hofu, katika kipindi hiki kilichojaa migogoro ya kibinadamu, yanaonekana kuongezeka kwa asilimia 20 kutoka asilimia 10 katika nyakati tulivu za nyuma . Hivyo inaonyesha idadi ya watu walioathirika na maafa ya kibinadamu imepanda duniani kote, na hivyo kuongeza mahitaji ya huduma katika afya ya akili. Ni maelezo yaliyotolewa na Inka Weissbecker, wa Kitengo cha kimataifa cha afya ya akili na mshauri wa kisaikolojia katika Shirika la Misaada la Kimataifa la Madaktari .
Watalaam wa afya walitoa maelezo wakilenga hali halisi za a afya ya akili za watu, kwenye nchi zilizokabiliwa na migogoro ya kivita kama vile Sierra Leone na Sudan Kusini . Na kwamba hadi hivi karibuni, wafadhili kwa mfano nchini Sudan Kusini, wanachukulia huduma ya afya ya akili kama huduma isiyokuwa muhimu. Na wametaja unyanyapaaji na ukosefu wa elimu kuwa vikwazo vikubwa katika ufanikishaji wa huduma za afya ya akili katika nchi zote, wengi hawajui kama magonjwa ya akili yanaweza ponyeka kwa matibabu, Dr Weissbecker alisema.
Na Mark van Ommeren, Mshauri wa afya ya umma wa WHO, juu ya masuala ya akili amesema: kuna takwimu za kutosha zinazoonyesha kwamba, kwamba, afya ya akili ni tatizo kubwa katika maisha ya wengi , kuliko hata ilivyokuwa siku za nyuma. Vita na majanga ya asili vimefungua mianya mingi inayoathiri akili ya mtu . Na hivyo ni muhimu kufungua pia mianya mipya safi kwa ajili ya huduma ya afya ya akili, kama kipengere muhimu pia katika kuboresha uchumi wa nchi na maendeleo ya jumla, alisema.
Nayo Matokeo ya Utafiti wa WHO yaliyochapishwa siku ya Jumanne, yanaonyesha kwamba kila dola moja inayowekezwa katika kutibu mfadhaiko wa akili huzalisha dola 4 zaidi kutokana na ufanikisha wa afya bora na uwezo wa watu kufanyakazi . Matibabu dhidi ya mfadhaiko wa akili unaotokana na hali za kuhuzunisha na wasiwasi yana faida zaidi katika maisha ya kijamii na kiuchumi pia kwa kuwa, huwezesha watu kufanya kazi zaidi . Utafiti huo umeonyesha mafanikio haya kwenye uhusiano wa karibu wa afya na faida ya kiuchumi kupitia uwekezaji katika matibabu, kama ilivyoonekana kwenye nchi 36 zenye kipato cha chini, kati na juu zilizohusika kwenye utafiti huu,ikiwemo Afghanistan na Sri Lanka , Burundi, mkoa wa Indonesia Aceh, Iraq, Jordan, Kosovo, Timor ya Mashariki, Lebanon na sasa Syria.
All the contents on this site are copyrighted ©. |