2016-04-12 07:16:00

Mkutano wa 14 wa Baraza la Makardinali washauri unaendelea!


Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 11- 13 Aprili 2016 anafanya mkutano na Baraza la Makardinali washauri. Huu ni mkutano wa kumi na nne unaofuatilia kwa kina na mapana mchakato wa mageuzi makubwa katika Sekretarieti ya Vatican! Tutakushirikisha yale yaliyojiri ndani na nje ya Vatican katika maisha na utume wa Kanisa. Itakumbukwa kwamba, mikutano mingine imefanyika kati ya tarehe 1- 3 Oktoba; 3- 5 Desemba 2013.

Kwa mwaka 2014 mikutano hii ilifanyika kati ya tarehe 17- 19 Februari; 27- 30 Aprili; 1- 4 Julai; 15- 17 Septemba na tarehe 9 – 11 Desemba. Kwa mwaka 2015, Baba Mtakatifu Francisko aliongoza mikutano ya Makardinali kati ya tarehe 9- 11 Februari; 13- 15 Machi; 8- 10 Juni; 14- 16 Septemba na tarehe 10- 12 Desemba. Kwa mwaka 2016 mkutano wa kwanza ulifunguliwa tarehe 9- 9 Februari 2016.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.