2016-04-03 09:32:00

Pd. John Akin Oyejola ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Osogbo, Nigeria!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre John Akin Oyejola, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Osogbo, Nigeria. Askofu mteule alizaliwa tarehe 8 Mei 1963, Jimbo Katoliki la Oyo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 5 Oktoba  1991 akapewa Daraja takatifu la Upadre. Tangu wakati huo, amekuwa ni Paroko msaidizi, Paroko, Mkurugenzi wa miito Jimbo; Mkurugenzi wa Utume wa Biblia Jimbo.

Kuanzia mwaka 1997 akatumwa na Jimbo kwenda kuongeza ujuzi na maarifa, Dublin, Ireland na kurejea tena nchini mwake kunako mwaka 1999 na kukabidhiwa Parokia kama Paroko. Akateuliwa kuwa ni kati ya washauri wa Jimbo. Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2010 akateuliwa kuwa ni Mkurugenzi wa elimu Jimbo. Katika kipindi hiki pia aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha shughuli za kichungaji Kikanda.

Baadaye akajiendeleza kwa masomo ya juu kuhusu familia huko Calfonia, Marekani. Akiwa masomoni alitoa huduma mbali mbali za kichungaji. Aliporejea nchini Nigeria, mwaka 2015 akapangiwa kuwa ni Paroko na mkurugenzi wa kituo cha Familia Jimbo la Oyo, nchini Nigeria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.