2016-03-22 14:00:00

Mwana Mfalme wa Luxembourg na Mkewe wamtembelea Papa Francisko


Jumatatu akiwa katika makazi yake ya Vatican , Papa Francisko, alimpokea Mwanamfalme  wa Luxembourg, Henri Albert Gabriel Felix Marie Guillaume na mke wake Maria Teresa Mestre.  Papa na wageni wake walifanya mazungumzo binafsi  katika hali ya  faragha kwa muda usiozidi nusu saa, Mwanamfalme akiwa na watoto wake watano na wake zao na wajukuu watatu.

Familia hii ya kifalme ya Luxembourg, ilitoa zawadi ya picha ya kuchorwa ya familia yenye maneno yaliyoandikwa katika lugha ya Kihispania "Kwa Papa wetu Francisko, kwa heshima ya upendo familia yetu yote." Nae Papa alitoa zawadi ya medali ya Kipapa na nakala ya waraka wake wa Kitume juu ya "Injili ya Furaha"(Evangelii Gaudium), na  hati ya Kitume juu ya utunzaji wa dunia na viumbe , Laudato si . Aliibariki familia hiyo na  pia kuiomba wamkumbuke pia katika sala zao.

Na wakati wa kuagana na Papa, Mwanamfalme alionyesha kutambua na kutoa shukurani zake  za dhati kwa Baba Mtakatifu,  kwa kila jambo analolifanya kwa ajili ya Kanisa zima la Ulimwengu. 








All the contents on this site are copyrighted ©.