2016-03-08 12:14:00

Mazoezi ya Kiroho kwa Papa Francisko na wasaidizi wake!


Jumatatu jioni Baba Mtakatifu Francisko na wasaidizi wake wa karibu wakiwa katika kituo cha kiroho cha Ariccia nje kidogo ya jiji la Roma, waliendelea kupata tafakari ya Neno la Mungu katika kipindi hiki cha kwaresima. Mhubiri akiwa Padre Hermes Ronchi, Mtawa wa Shirika la Watumishi wa Maria. Madhari ya mafungo imeelekezwa katika mswali ya Yesu. Baada ya kutoa tafakari katika maswali "Mnamtafuta nani", na "kwa nini mnaogopa",  tafakari ya tatu ililenga katika swali “iwapo chumvi itapoteza ladha yake kwa vipi itakoleza chakula”? (Injili ya Mathayo).

Padre Ronchi alileza kwa kina thamani ya chumvi tangu ulimwengu wa kale ambao inaendelea kuwa kiungo muhimu hata sasa katika shughuli za kulete ladha na hifadhi na hivyo katika maisha ya binadamu ni moja ya bidhaa  muhimu inayotakiwa kuwepo na hutuzwa daima. Ndiyo maana Yesu aliutumia mfano wa chumvi akilinganisha na mitume wake  katika kudumisha maisha matakatifu na neno la Mungu duniani. Padre Ronchi amesema Mitume kama chumvi , walipaswa  kuhifadhi  uhai wa Neno la Mungu na Injili duniani , wakipenyeza na kuvidumisha . Chumvi ya dunia na Nuru ya ulimwengu, anaendelea kusema Yesu  katika Injili  kwamba ni unyenyekevu katika kulipokea neno na kulitumia kukoleza yaliyo mema katika jamii , na hivyo ni  mfano wa kuigwa na Kanisa na wanafuasi wake.  

Aliendelea kufafanya juu ya  unyenyekevu wa chumvi na mwanga, pale vyenyewe vinapokosa ubora wake ,  jinsi chumvi inavyopoteza thamani yake iwapo inapoteza ladha yake. Amekuita kupoteza huko kwa ladha kuwa sawa na wafuasi wa kanisa ambao tabia zao hazionyeshi  tabia za Kristo, tabia za majivuno na ubabe, wanakuwa wamepoteza  hupoteza radha hiyo.

Pia akasema, haisaidii chochote kuwa na chumvi iliyofungiwa katika chupa bila kutumiwa koleza chakula jikoni.  Kama yalivyo madhumuni yake,  chumvi  huwa na faida tu pale inapotumika. Na vivyo hivyo kwa wafuasi wa Yesu, haifai kuamini na kujifungia imani hiyo ndani ya mtu mwenyewe,  bila kuipeleka kwa watu wengine. Yesu anapenda wote wanaomwamini pia waifikishe furaha yao ya kuwa na Yesu kwa watu wengine, walio bado kukutana na Yesu. Ni lazima kwenda nje na kuwapata waliopotea na  kufanya mambo mema zaidi.  Amehimiza waamini na wachungaji wao kwa pamoja kama Kanisa ni lazima kutoka na kwenda nje ,  kulihubiri Neno la Mungu, Wokovu wa Bwana , kwa  unyenyekevu na matendo mema ili watu wapate kusadiki, onjo hilo la uzuri wa neno la Mungu lionekana kukoleza maisha mazuri kama chumvi iongezavyo ladha katika chakula  na kama nuru inayofukuza giza nyakati za usiku. Ameonya  kwa kuifunga na kufuli nafsi, hata kama inapambwa na fadhila zote nzuri zaidi, kama hakuna mawasiliano na wengine, ni sawa na chumvi iliyopoteza radha. Ni sawa na mwanga uliowekwa chini mvunguni.  Na hivyo  kuwa muumini mzuri wa Kanisa si tu kuzishika amari za Mungu na kanisa lakini ni kutoka na kujiunga katika njia ya kutenda mema na kufanikisha maisha mazuri kwa watu wote.

Padre Ronchi ameonya dhidi ya muumini kuwa na woga na hofu, kwa kuwa hali hiyo  huwa na mwelekeo wa kupoteza ladha, inakuw ani imani ambayo bado kufufuka kiimani. Bado kuwa huru dhdi ya uso wa hofu na woga.Na kwamba Yesualionya mara kwa mara watu walipenda kukutana na Yesu aliye hai na si wingi wa mafundisho magumu na sheria . 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.