2016-02-22 14:46:00

Papa awataka wafanyakazi wa Curia na Vatican kuwa watu wa huruma


Mkiwa Wafanyakazi wa Vatican na Ofisi za Jimbo Takatifu , ni lazima kila siku kuruhusu huruma ya Mungu itende kazi  ndani ya mioyo yenu, na katika kuwa mashahidi wa manufaa  ya kukiri imani kwa  Kristo. Ni Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Jumatatu hii,  wakati akiongoza  Ibada ya Misa kwa ajili ya Mwaka Mtakatifu wa  Jubilee ya Huruma ya Mungu kwa Wafanyakazi wa Idara za Curia ya Roma na Taasisi zote za Vatican.  Kabla ya Ibada , wafanyakazi hao waliandamana na Baba Mtakatifu tokea  Ukumbi wa Paulo VI na kupita katika Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kukusanyika katika  Madhabahu ya Kuu ya Kaburi la Mtume Petro kwa ajili ya kikukiri imani yao .  Papa kwa namna ya kipee aliombea  utendaji wao,  uangaziwe na Neno la Mungu,  wakifuata mfano wa Mchungaji Mwema ,  katika kuliongoza Kundi la  Kristo,  yaani Kanisa. .

Homilia ya Papa alilenga katika uthabiti wa kuikiri imani , akitazamisha katika swali la Yesu  "Na ninyi je, mwasema mimi ni nani? (Mt 16:15)”. Swali alilolitaja kuwa ni swali wazi na  la moja kwa moja, ambalo si rahisi kulikwepa nahalina ugumu katika kutoa jibu. Na hivyo alimtaka kila mmoja, ndani ya moyo wake, kutoa jibu  kwa uaminifu. Alisema Yesu hakuuliza swali hili kw ania za udadisi tu, lakini  kama swali  msingi lenye kuonyesha upendo kamili wa Yesu! Ni swali linalomtaka Mkristo kuonyesha hali y aimani yake kwa Kristo. Imani yenye  kuonyesha kumtambua kuwa  Kristo kuwa  ndiye Mwana wa Mungu na Bwana wa maisha. Papa amesemani  wito mpya na wa kwanza katika kuikiri imani, na hasa kwa  kazi za mwandamizi wa Petro,  ambaye hawezi tangamana na  jukumu la kuwaimarisha nduguzake katika Kristo Lk 22:32).

 Baba Mtakatifu Francisko aliendelea kuwataka wafanyakazi wa Vatican na idara zake , kuachia neema za Mungu , kuunda upya mioyo yao katika imani na kufungua midomo yao na kudumu katika  kuiugama imani na  wokovu waliopokea(Rum 10:10). Na hivyo wote wanapaswa kujibu kama Mtume Petro :  "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mt 16:16). Kwa hiyo mawazo yao na macho yao na utendaji wao wote , vinatakiwa kuitazama sana sura ya Yesu Kristo, aliye mwanzo na mwisho wa kila shughuli ya Kanisa.  Yeye ni jiwe la msingi  la kazi zote za Kanisa na hakuna mtu anayeweza tengua ukweli huo na maelezo tofauti (1 Wakorintho 3:11). Kristo ndiye "mwamba" ambayo ni lazima kazi zote za Kanisa kujenga juu yake.

Aidha Papa alikumbusha  maana ya maneno ya Mtakatifu Augustine anapoandika  juu ya misukosuko,  machafuko na matukio ya kihistoria akisema kwamba havikulizima Kanisa, kwa kusababu Kanisa limejengwa juu ya mwamba ambao  Petro aliitwa kw ajina hilo. Ni mwamba ambao Petro alipata uimara wake na si mwamba ulichota uimara wake toka kwa Petro,. Na ndivyo kwa namna hiyo hiyo, kwamba Kristo jina lake halitokani na Mkristo lakini Mkristo hupata jina lake kutoka kwa Kristo. Mwamba ni  Kristo, msingi wa ambao juu yake  Petro, analijenga Kanisa la Kristo(Yn 124, 5: PL 35, 1972).

Baba Mtakatifu aliendelea kuzungumzia haja ya kila mmoja  kukiri  imani  yake kwa uthabiti, kama wajibu kwa  kila aliyeitwa katika huduma za Kanisa, na hasa kwa Wachungaji, juu ya yote, wanatakiwa kuishi kama mfano wa Mungu mwenyewer ambaye huliongoza kundi lake, kama Nabii Ezekieli  alivyoutaja utendaji wa Mungu kwamba: Yeye huenda katika kutafuta kondoo waliopotea,huwageukia wale walioumizwa au kujeruhiwa kiroho kuwatibu magonjwa yao Hiyo ndiyo tabia anayotakiwa kuwa nayo mchungaji , kuwa na  huruma isiyokuwa na mipaka. Kuwa mchungaji ni majitoleo katika kina cha imani tena  mara kwa mara, bila masharti, kwa sababu wote ni dhaifu wenye kuhitaji kuifikia huruma ya Mungu.Alieleza kwa kurejea tena utabiri wa Nabii Ezekieli , kwa viongozi wa wana wa Israel,ambamo aliwataka viongozi hao kwanza waanze kujichunguza mapungufu yao wenyewe.  Na ndivyo ilivyo kwa  , aliyeitwa kuwa Mchungaji katika  Kanisa, kwanza aruhusu kuangaziwa na  uso wa Mungu Mchungaji Mwema, kuruhusu kusafisha nae na ubadilisha  maisha kwa kufanya ukarabati kamilifu wa dhamira, ili  kwamba hata katika mazingira ya  kazi, waweza kusikia kwa nguvu, wito wao wa kuwa wachugaji , hasa kwa watu wanaokutana nao siku hadi siku, ili kwamba kusiwe na mtu anayejisikia kupuuzwa au kutendewa vibaya, lakini kila mtu aweze  kuishi kwa furaha ya kuwa karibu na mlezi wenye  upendo wa Mchungaji Mwema.

Papa amewaambia kwamba, wao daima wameitwa kuwa  washirika wa Mungu katika kufanikisha kazi yake muhimu na ya kipekee ya kuwa  shahidi wa nguvu wa neema ya Mungu yenye kubadilisha maisha kwa nguvu za Roho anayeleta  upya.

Baba Mtakatifu alieleza na kumtaka kila mmoja amwachie Bwana amwokoe dhidi ya  kila jaribu, linalotaka kumweka mbali  na dhamiraza kumtumikia Bwana, na katika kugundua upya uzuri wa kuikiri imani  kwa Bwana Yesu Kristo.  Aliongeza uaminifu katika utendaji wa kazi huenda sambamba na huruma ya Mungu,  tunayotakiwa kuiishi kila siku.  Na kwamba katika Maandiko Matakatifu, kwa hakika, uaminifu na huruma haviwezi kutenganishwa, ni mambo yaliyoshikamana pamoja. Mahali palipo na uaminifu pia kuna huruma, ni mambo yaliyoungana yanayo onyesha uwepo wa sura ya Mchungaji Mwema. Alikumbusha, uaminifu unahitaji kutenda kwa mujibu wa moyo wa Kristo. Kama Mtume Petro alivyosema ,  ni lazima kulisha kundi kwa roho ya ukarimu" na kuwa "mfano" kwa wote, ili wakati Mchungaji Mkuu  Mwema atakarudi, wawe na uwezo wa kupokea "taji ya utukufu isiyonyauka “ (1Pet 5:14).
 








All the contents on this site are copyrighted ©.