2016-02-16 14:54:00

Askofu mwandamizi George Bugeja ateuliwa kuwa msimamizi wa kitume Benghazi


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Sylvester Carmel Magro, O.F.M. Msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Benghazi, Libya kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401§ Ibara ya 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu mwandamizi George Bugeja, O.F.M kuwa Msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Benghazi, Libya na kuendelea pia kuwa msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Tripoli, Libya. 

Askofu mwandamizi Bugeja alizaliwa kunako tarehe 1 Julai 1962 huko Malta. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa kunako tarehe 28 Agosti 1983 akaweka nadhiri za daima. Tarehe 10 Juali 2015 akateuliwa kuwa Askofu mwandamizi wa Tripoli, Libya na kuwekwa wakfu hapo tarehe 4 Septemba 2015. Tarehe 14 Februari 2016 akateuliwa kuwa Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki Benghazi, Libya.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.