Mamia ya Wakatoliki na wasio Katoliki wa Jimbo Kuu la Mbarara, mwishoni mwa wiki walisongamana katika Kanisa Kuu la Nyamitanga wakiongozwa na Askofu Mkuu Paulo Bakyenga , kutoa heshima zao za mwisho na mazishi ya Askofu Mstaafu John Baptist Kakubi wa Jimbo Kuu la Mbarara. Askofu Mstaafu Kakubi alifariki dunia Alhamis ilyopita katika Hospitali ya Kimataifa ya mjini Kampala, akiwa na umri wa miaka 87.
Ibada ya Misa ya Wafu , iliongozwa na Askofu Mkuu Paul Bakyenga katika Kanisa Kuu la Nyamitanga na baadaye ibada ya mazishi katika Kanisa dogo la Kituo cha Malezi ya Kiroho cha Mtakatifu Yosefu kwa matashi yake Marehemu. Kituo alichokianzisha ambacho alikuwa akivunia uwepo wake wa miaka 35 kuweza kutoa matunda ya watalaam wengi wa ngazi za juu , wakiwemo mapadre, madaktari na wanasheria.
Maaskofu wengine waliohudhuria maziko haya ni pamoja na Askofu Vincent Kirabo wa Jimbo la Hoima Askofu John Baptist Kaggwa wa Jimbo la Masaka, Askofu Callist Rubaramira wa Jimbola Kabale Askofu , Robert Muhirwa wa Jimbol a fort Portal Askofu Egidio Nkaijanabo wa Jimbo la Kasese, Askofu Lambert Bainomugisha Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Mbarara naAskofu Mstaafu Edward Baharagate wa Jimbo la Hoima. Pia walihudhuria viongozi wa makanisa na mani zingine akiwemo kutoka Dayosisi ya Kianglikani ya Ankole Askofu Sheldon Mwesigwa, pia Kadhi wa Wilaya wa Mbarara, Sheikh Ramadhan Khamis na mtangulizi wake Sheikh Abdu Noor Kaduyu. .
Askofu Bakyenga , katika homilia yake alimtaja Marehemu Askofu Kakubi kuwa mfano wa kuigwa na viongozi wa kanisa, waamini na watu wote katika kuwa mtu mpole na adilifu. Kwamba alikuwa ni mtu mwenye bidii katika maombi, na mwenye kujituma.
Habari zake binafsi zinasema, alizaliwa Septemba 23, 1929, kijijini Kyanda, Rugaaga, Parokia ya Birunduma ambayo sasa ni Wilaya ya Isingiro. Alisoma Shule ya Msingi ya Birunduma na Nyamitanga na semnari ndogo ya Kitabi Bushenyi, na baadaye Seminari kuu ya Katigondo Masaka, na St Edmund ya Allen Hall, Uingereza.
Baada ya kupadirishwa alifanya utume wake katika Paroliki ya Nyamitanga, kisha Seminari ya Kuu ya Katigondo na Kitabi . Aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mbarara Julai 5 1969 na Septemba 7, 1969 alsimikwa kuwa Askofu wa Mbarara. Mwaka 1980, alianzisha Shule za Malezi za Mtakatifu Yosefu na Cha Mtakatifu Cecilia
Alistaafu kazi za kichungaji za jimbo mwaka 1991, bada ya kutumikia kama Padre kwa miaka 55 na 47 kama Askofu. Mungu ailaze Roho yake pema Peponi.
All the contents on this site are copyrighted ©. |