2016-02-10 15:11:00

Jubilee ni wakati wa huruma na msamaha.


Katekesi ya Baba Mtakatifu kwa mahujaji na wageni, Jumatano tarehe 10 Febnruari 2016 imetazama kwa kina  maana ya mwaka wa Jubilee , ikiangalisha katika mafundisho ya kidini  kama ilivyoandikwa katika Agano la kale, na kutoa wito wa kuwa wasamehevu , kupambana na umasikini na kujenga usawa  katika matumizi na mapato ya mali asili za dunia kwa manufaa wote.  

Baba Mtakatifu alieleza kwa kufanya rejea katika Kitabu cha Mambo ya Walawi, akisema, Maandiko Matakatifu yanatufunza kwamba,  mwaka wa Jubilee ni maadhimisho ya  maisha ya kidini na kijamii ya tangu kale , kwamba ni wakati wa kusamehe waadeni na watumwa kuachiwa huru. Kwa hiyo mwaka wa Yubilee ni mwaka wa msamaha kwa  ujumla. Ni wakati kwa watu  wote kurejea katika  asili ya uadilifu ,  na uhuru kamilifu  kama  taifa takatifu la Mungu.

Baba Mtakatifu ameeleza na kuomba uvuvio wa Roho Mtakatifu , uweze kuwaongoza watu hasa matajiri ambao  wengi wao, akili yao husumbuka kufikiri juu ya vitu vingi alivyo navyo , wafanye nini navyo.  Papa amewataka wasipate tabu nam ali zao bali wavitoe  kama sehemu moja ya kumi, watu maskini wasiokuwa na kitu.  

Papa amemtaka kila mmoja kujichunguza mwenyewe  moyo wake na kujiuliza ana vitu vya ziada anavyopaswa kuvitoa kwa watuwengine. . Kwa uwepo a Jubilee Papa anasema , ni wakati kwa wale wasiokuwa na kitu kuweza kupata mahitaji yao ya lazima katika maisha na kwa waliokuwa matajiri kurudisha kile walichokipokonya kwa maskini, ili hatimae kujenga jamii yenye usawa na mshikamano, kwa manufaa ya wote.

Maoni ya papa yalilenga pia katika taarifa za hivi karibuni zinazoeleza kwmaba , asilimia themanini ya utajiri wa dunia uko katika mikono ya asiliamia 20 ya watu wote duniani. Kwa maoni hayo , Papa aliendelea kufundisha kwamba, tunapaswa kuutumia muda huu wa  Jubilee ya huruma ya Mungu, kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa kwa kukuza mgao sawa wa utajiri wa dunia kwa manufaa ya wote.  Ardhi ni mali ya  Mungu, iliyokabidhiwa kwetu sisi binadamu , ambao si kitu lakini wageni  na wasafiri katika njia inayoelekea umilele.  Na kama mawakala wa Bwana ,tunaitwa  kuishi na kuiheshimu dunia  tuliyokabidhiwa na kuipokea. Na kwamba iwapo maadhimisho haya ya Jubilee ya huruma hayagusi mifuko yetu basi hi isi kweli ya kweli.

Papa anasema , haya ni mafundisho ya Biblia na si mafundisho ya Papa binafsi. Mtazamo wa Mafundisho ya Biblia kwa Jubilee ni  yanalenga katika kujenga jamii iliyosimikwa katiakmingi ya kufanikisha usawa  na mshikamano , mahali ambamo uhuru na fedha vinakuwa ni kwa manufaa ya wote na si kwa ajili ya watu wachache.

Hivyo katika mwaka  huu Jubilee,  tuna changamotishwa  na Maandiko Matakatifu , kutoa kwa ukarimu zaidi , moya ya kumi ya mapato ya kazi zetu, bila kufikiri fikiri faida za ziada.  Na kwamba, daima ni jambo jema kuwanasua wenzaku wanaokabiliwa na umaskini na matatizo yenye kuwanyima  mahitaji ya lazima kimaisha. Ni vyema kuwasaidia wote bila kujali kama twawafahamu au la, bali kusaidia kama wajibu kwa mtu wa  Mungu.  

Papa alihitimisha Katekesi yake kwa kukumbusha adhimisho la Siku Kuu ya Mama Yetu wa Lourdes ambayo pia ni adhimisho la 24 la Siku ya Wagonjwa duniani, akiomba waamini wote wakumbe kuwaombea wagonjwa wote faraja  toka kwa  Mwenyezi Mungu. 








All the contents on this site are copyrighted ©.