2016-02-01 07:37:00

Siku ya Wagonjwa wa Ukoma Duniani: 'Kuishi ni kuhudumu maisha"


Jumapili tarehe 31 Januari, ilikuwa ni  Siku ya Wagonjwa wa Ukoma Duniani, ambayo huadhimishwa kila  mwaka ,  Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari. Siku hii iliwekwa kwa lengo la kuhamasisha upya dunia kutazama kwa makini zaidi, juhudi za kutokomeza ugonjwa wa ukoma duniani kote. Siku hii ilianzishwa tangu mwaka 1954 na  Mfaransa, Mtalaam wa vijidudu vinavyosababisha maradhi mwilini na akiwa pia mwandishi, Raoul Follereau, kama njia ya kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huu mbaya wa tangu zama za kale.

Askofu Mkuu Zygmunt Zimowski, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma za Kichungaji kwa Wafanyakazi wa Afya , kwa ajili ya Siku ya Wagonjwa wa Ukoma Dunia likiwa ni adhimisho la 63, ametoa ujumbe wake chini ya Mada:  ”Kuishi  ni kusaidia kuishi”. Ameitaja siku hii kuwa  ni fursa kwa kila mmoja,  kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi  ya ugonjwa huu wa kutisha  na kutokomeza unyanyapaaji wenye kusababisha mara nyingi hali ngumu zaidi kwa wale wanao onekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.  

Ujumbe wa Askofu Mkuu , unakemea tabia za kuwabagua au kuwanyanyapaa wagonjwa w ukoma katika maisha ya kawaida ya kijamii, akiongeza kwamba, pamoja na hisia za kujikinga dhidi ya ugonjwa huu usioponeyka kwa haraka, leo hii hakuna sababu za kuwa woga kiasi hicho kwa kuwa ukoma kwa sasa unaweza tibika. 

Anasema kuwatenga wagonjwa wa ukoma  katika maisha ya kijamii, husababisha mateso zaidi kwa watu hao ambao wamejikuta katika hali ya kushambuliwa na vijidudu hao wenye kuleta majeraha  na ulemavu wa kudumu mwilini. Kwa maana hii, wale walio katika hali ya afya hii teke wanapaswa kusaidiwa kuishi maisha ya hadhi na stahili badala ya kuwanyanyapaa na kuwatenga katika haki za kijamii. .

Askofu Zimowski , amesisitiza na kutaka uwajibikaji zaidi na mshikamano uliosimikwa katika pendo wa kidugu  na huruma, kama, inavyotakiwa katika maadhimisho ya  Mwaka Mtakatifu wa  Jubilee ya Huruma , ambamo Papa Francis anafundisha na kuhimiza kwamba ni lazima kwa Mkristo kuishi  kwa ushuhuda wa matendo ya huruma kwa wengine na hasa kwa wahitaji zaidi. Ni kuwa na jicho la ubinadamu na huruma   si hofu kwa yale yanayotokea. Ni lazima kuziishi ishara za Huruma ya Mungu ambaye ni Upendo .

Ujumbe wa  Askofu  Mkuu Zimowski unaendelea kutazama pia ujumbe  wa Papa Francisko kwa ajili ya adhimisho la Siku ya Siku ya Wagonjwa Duniani hapo tarehe  Februari 11 , ambamo Papa anatafakri juu ya huduma ya Mama Bikira Maria katika  huruma Mungu, akisema kwamba,   unyenyekevu wa Bikra Maria unapaswa kuwa katika  maisha ya watu wote wale wanaowahudumia wagonjwa na kuelewa mahitaji yao, hata yale yenye kudai zaidi, kwa sababu wagonjwa wanahitaji huruma na upendo kamili wa kina.

Askofu Mkuu Zimowski, anaendelea kutazama upande wa Kanisa na kusema , ni dhamira ya Kanisa kusaidia  matibabu ya wagonjwa wa ukoma na kutoa msaada kwa wale wanaopona,pamioja na juhudi za kuelemisha umma juu ya ugonjwa huu. Kwa mtazamo huo, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma za Kichungaji kwa wafanyakazi wa Afya , kwa kushirikiana na Shirila la Sasakawa  na shirika la  Raoul Follereau, limeandaa mkutano wa siku mbili mwezi June 10 na 11 hapa Vatican., Mkutano utakaohitishwa na Ibada ya MIsa itakayoongozwa na Papa Francisko katika uwanja wa  Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,  hapo tarehe 12 Juni, kama sehemu ya Maadhmisho ya Jubilee ya mwaka Mtakatifu wka wagonjwa na walemavu.

Askofu Mkuu Zimowski amekamilisha ujumbe wake kwa  kukabidhi  maadhimisho ya hii Siku ya Wagonjwa wa Ukoma Duniani kwa Mama Bikira  Maria,  ili tuweze kuchukua hatua  zinazoweza kuivusha mioyo yetu dhdi ya kwuanyanyapaa wagonjwa wa Ukoma , wakati tunapopita katika Mlango Mtaktifu wa Huruma yamungu na kukutana  kwa furaha na kila mmoja  katika furaha ya kweli ya  maisha. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.